Unknown Unknown Author
Title: JACKILIN WOLPER ANENA KUWA "ZAMARADI MKETEMA MNAFIKI NA NI ADUI YANGU NAMBA MOJA", PATA UNDANI HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hali ya maelewano kati ya muigizaji wa bongo movie Jacqueline Wolper na mtangazaji wa kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds TV na Clouds FM, Za...

clip_image001[8]Hali ya maelewano kati ya muigizaji wa bongo movie Jacqueline Wolper na mtangazaji wa kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds TV na Clouds FM, Zamaradi Mketema inaonekana kuwa si nzuri baada ya Wolper kumshutumu mtangazaji huyo akidai kuwa amekuwa akimfuatilia sana katika mambo yake binafsi.

clip_image001[10]Wolper amezungumza hayo alipohojiwa na gazeti la Amani, na hivi ndivyo habari hiyo yenye kichwa cha habari ‘Wolper, Zamaradi bifu zito’ ilivyoandikwa kupitia mtandao wa Global Publishers.

STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.

Akizungumza na Amani juzikati, Wolper alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa mtindo wa hasi (negative), akamuomba amuache.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.

“Huko nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi karibuni) kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu.

Naomba niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha yangu,” alilalama Wolper.

Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.

clip_image001[6]“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top