Msanii kutoka TMK Wanaume Family Chege Chigunda anatarajia kuupokea mwaka mpya kwa kutoa video mbili kwa wakati mmoja. Video hizo ni za single yake mpya ‘Chapa Nyingine’ aliyoitoa hivi karibuni pamoja na single yake nyingine ya miondoko ya Reggae inayoitwa ‘Binadamu’.
CHEGE CHIGUNDA “MTOTO WA MAMA SAIDI”
Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fella, amesema kuwa video ya ‘Chapa Nyingine’ imefanyika Tanzania chini ya director wa Visual Lab/Next Level Adam Juma, huku video ya Binadamu ikiwa imefanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Video.
“Video zote mbili za Chegge zitatoka kwa mara moja ule usiku wa mkesha wa mwaka mpya, hii single yake ya sasa na Binadamu. Ile Binadamu ni Reggae…audio yake iliwahi kutoka kimakosa ndio maana huisikii hata Redioni so tunafocus zaidi kwenye video ” alimaliza Fella.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.