WAKAZI WA MJI WA LINDI WAKOSA HUDUMA SIKU MBILI MFULULIZO

mgomo lindi (9)Na Abdulaziz Video
Wakazi wa Manispaa ya Lindi Wameendelea kukosa huduma ya kununua bidhaa za madukani ikiwemo vyakula kwa siku ya pili mfululizo kufuatia mgomo ulioitishwa na wafanyabiashara kutokana na kodi kubwa inayotozwa na mamlaka ya mapato ikiwemo kodi ya huduma inayotozwa na halmashauri ya manispaa ya Lindi
mgomo lindi (6)Kufuatia mgomo huo wafanyabiashara hao walikutana katika ukumbi wa Double M hotel na kuazimia kuendelea na mgomo hadi wenzao
waliofikishwa mahakamani kwa ajili ya kodi ya Huduma kuachiliwa
mgomo lindi (12)Taarifa zaidi ya Mgomo huo na hatua zilizochukuliwa tutawajuza baada ya Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao,Hamis Livembe atakapotoa taarifa baada ya uongozi huo kukutana na Kamanda polisi kikao ambacho kinaendelea sasa…

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post