Nafasi ya Pekee: Robin van Persie akikosa penalt ya pili akiwa na Manchester United
Robin van Persie amekosa penalt ambayo ilipatikana baada ya ashley young kuchezewa ndivyo sivyo kwenye eneo la hatari na Javier Hernandez alikosa nafasi ya wazi na kupaisha mpira juu ya goli baada ya kupokea pasi maridadi iliyopigwa na Kagawa na kufanya matokeo ya mchezo huo kwenda Suluhu hadi mwisho wa mchezo.
TAHARUKI: Javier Harnandez akipaisha mpira juu ya goli mita chache nje ya sita, alitakiwa kufunga
Vijana wa David Moyes's walitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo zingewapa ushindi leo hii lakini hawakuzitumia ipasavyo hatari zaidi ni kwa mchezaji Marouane Fellaini kupatiwa kadi nyekundu nakutolewa nje.
Van Persie pia aligogesha mwamba wa pembeni na kukosa kufunga goli ambalo lingeipa point tatu Manchester united dhidi ya wahispania Real Sociedad.
AKIANGUKA CHINI: Ashley Young aanguka chini baada ya kushikwa na mchezaji wa Real Sociedad.
Mchezaji huyu wa Manchester United amekuwa na rekodi ya kujiangusha hasa katika eneo la hatari kama alivyofanya leo dhidi ya Sociedad na kupewa penalty.
SIBAHATI: Van Persie Akigonga mwamba wa pembeni katika harakati za kutafuta goli.
Juu Juu nakuondoa mbali: Marouane Fellaini akipiga kichwa kuokoa hatari langoni mwa timu ya Manchester United
MATOKEO KWA UJUMLA
| | |
| |
| | |
| |
| | |
| |
| København | 1 | | | Galatasaray | 0 | | |
All times are in Tanzania Time