TUZO YA MWANGOSI APEWA ABSALOM KIBANDA

DU7A0225Na Abdulaziz video,Mwanza
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari akabidhiwa Tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka - iliyofanyika Mwanza Jana.

Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda jana
amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya
Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka huu.
kibandaKabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.

Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza baada ya makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa.DU7A9903Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini.DU7A9916Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi
millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za vitisho.

Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii.

Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post