Wananchi wa Vijiji Vya Singino wilayani Kilwa mkoani Lindi
wamelalamikia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC )kwa kitendo cha kutokusimamia vyema kazi iliyopewa na Bodi ya Korosho Tanzania katika zoezi la uteketezaji kemikali zilizotelekezwa kwa zaidi ya miaka 20 zinazosadikika kuwa sumu inayoweza kuathiri afya ya binadamu, mifugo na mimea.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Diwani wa kata ya Kivinje, Jafari Arobaini na Mwenyekiti wa kijiji cha Singino Maulidi Mbulula walisema kitendo cha mkandarasi kumwaga ovyo dawa hizo kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi, mifugo na mimea na kuathiri kukua kwa mji huo.
Pamoja na zoezi hilo kusimamiwa na watu wa mazingira lakini bado
zoezi linaonyesha kutotekelezwa kama lilivyopangwa katika makubaliano ya pamoja kati ya serikali ya kijiji, halmashauri, na NEMC Baada ya kukutwa kemikali hizo zikiwa zimemwagika njiani.
Kufuatia hali hiyo FAHARI YA KUSINI BLOG ilifika Katika ofisi ya Halmashauri kujua utaratibu unaotumika kuteketeza kemikali hizo zilizokuwepo katika Ghala la Korosho Kilwa, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Daniel Lisingu alieleza Bakari Mussa Mkazi wa kilwa Masoko ambae alipata kazi katika ghala hilo alieleza athari alizoziona na kuachia kazi hiyo kulinda afya yake huku Abdu Saidi mjumbe wa Singino ameomba uongozi wa wilaya kusimamisha zoezi ili kunusuru maisha ya wananchi wa eneo hilo kutokana na ukiukwaji unaoonekana sasa kazi inavyoendelea.
Kwa upande wake Afisa msimamizi mazingira NEMC Jorome Kayombo alisema kuwa awali NEMC ilimwagiza mkandarasi kuchimba shimo futi tano na kutandika kapeti chini, pembeni na juu ili kuzuia mwingiano wa kemikali hizo na udongo huku akikataa kupigwa picha na kutoa ufafunuzi zaidi wa kemikali hizo kwa madai si msemaji wa NEMC.
Katika hali isiyo ya kawaida Uongozi wa ghala hilo ulimwamuru mlinzi
kutoruhusu waandishi kuingia kuangalia hali ya utoaji wa madawa hayo ghalani kufuatia malalamiko ya vibarua wanaofanya kazi hiyo hatarishi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.