MTOTO WA BECKHAM AITEMA MAN UNITED NA KUTUA FULHAM

clip_image001Majaribio: Brooklyn amefanya majaribio na Fulham U-15

KINDA Brooklyn Beckham amepiga hatua nyingine katika harakati za kufuata nyayo za baba yake, kwa kufanya mazoezi na Fulham.

Beckham mkubwa amestaafu rasmi soka Mei mwaka huu, lakini sasa mtoto wa kiume wa David mwenye umri wa miaka 14 anaweza kuendeleza jina la baba yake katika soka.

Kinda huyo aliongozana na mama yake, Victoria kwenda kucheza mechi katika Uwanja ambao milango ilifungwa akiichezea timu ya vijana ya Fulham chini ya umri wa miaka 15 dhidi ya Southend jana.

clip_image002Familia: Beckham akipozi na watoto wake wa kiume, Brooklyn (kushoto), Cruz (katikati) na Romeo wakati anacheza LA Galaxy

Beckham ataendelea kufanya mazozei Motspur Park HQ, Uwanja wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ulio karibu na nyumbani kwao.

Kijana huyo ameonyesha nia ya dhati ya kufuata nyayo za baba yake kwa kufanya mazoezi na klabu nyingine kadhaa England, ikiwemo timu ya zamani ya baba yake, Manchester United mwezi uliopita ambako aliwavutia makocha wa akademi.

Beckham mdogo pia amefanya mazoezi na Chelsea na Queens Park Rangers mwaka huu.

clip_image002[5]Kama baba, kama mwana: Beckham akizungumza na Brooklyn katika mazoezi ya Real Madrid mwaka 2005

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post