Unknown Unknown Author
Title: HAYA NDIO MAJIBU YA JOH MAKINI KUHUSU SHOW YA P-SQUARE LIVE IN DAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ambaye aliungana na wasanii wa kundi la Weusi Jumamosi (November 23) na kudondosha show kali na kulipamba tam...

clip_image002Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ambaye aliungana na wasanii wa kundi la Weusi Jumamosi (November 23) na kudondosha show kali na kulipamba tamasha la ‘P-Square Live In Dar’, ameeleza vitu alivyojifunza kwenye performance ya wasanii hao ndugu toka Naija, Peter na Paul.

Joh ameiambia tovuti ya Times fm kuwa amejifunza zaidi jinsi ya kuwasiliana na audience wake wakati anaimba jukwaani na kuwafanya wawe wajisikie kuwa sehemu ya show.

“Kitu ambacho nimejifunza ni kwamba kuendelea kuongeza confidence na jinsi ya ku-communicate na fans unapokuwa jukwaani ndio kitu kikubwa zaidi kwenye show mbali na muziki unaokuwa unaufanya pale. Kuongea na watu na kuwacheck wako kwenye mood gani na kurelax kwenye stage ndio kitu ambacho nimejifunza. Kwa sababu hata ukiangalia show ya P-Square utagundua wao wana confidence wanapokuwa kwenye jukwaa wanaongea na watu. Inawafanya fans wanajisikia wako na wewe kwenye lile tukio sio tu unapiga wimbo baada ya wimbo unaondoka.” Ameeleza kaka yake Nikki wa Pili.

Akasisitiza, “Kwa hiyo communication kati ya msanii na mashabiki ni kitu muhimu sana na ndio kitu ambacho ninaendelea kujifunza kila siku kwenye show zangu.”

Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu maoni ya Joh Makini kwa upande wake kwa jinsi alivyoiona show hiyo kwa kulinganisha na show nyingine zilizowahi kufanyika Tanzania, kama hiyo anaweza kuiita ‘show bora zaidi’ kati zote alizowahi kuona za kimataifa hapa Tanzania.

“Kiujumla tamasha lilikuwa kubwa, na ni one of the biggest shows ambazo nimeziweka kwenye historia yangu. Performance yao ilikuwa nzuri lakini naamini kwamba tunaweza kufanya bigger than that kama tukiwezeshwa vizuri financially.” Amefunguka Joh Makini.

Joh amedai kuwa show hiyo haikumshangaza kwa kuwa anaamini kuwa walistahili kufanya vizuri hata zaidi ya walivyofanya kutokana na treatment wanazozipata kama wasanii wa kimataifa.

“Kwa hiyo sijashangaa, yaani hawajafanya kitu cha kunishangaza kwa kuwa naamini kwamba wanalipwa vizuri. kwa hiyo walistahili kufanya kile kitu walichokifanya kutokana na jinsi ambavyo wanapewa treatment kama wasanii wa kimataifa. Na nilitarajia labda watafanya hata zaidi ya kile ambacho nilikiona kutokana na treatment ambayo wanapewa kama International artists.

“Kwa hiyo nilichokiona pale ni kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi ya tulivyofanya, ama hata zaidi ya wasanii wengi wa kimataifa kama tutawezeshwa.” Ameeleza Joh Makini.

P’ Square walipewa kampani ya kutosha na wasanii wa hapa nyumbani Tanzania, Lady Jay Dee, Ben Pol, Joh Makini akiwa na kundi la Weusi na Profesa Jay.

SOURCE: TIMESFM.CO.TZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top