BALOZI WA PEPSI KALA JEREMIAH KUJA NA “WALEWALE”.

KALA JEREMIAHMkali anayefanya vizuri kwenye anga za HIP HOP ndani ya TANZANIA, ambaye alifanikiwa kutwaa tuzo ya msanii bora wa Hip Hop 2013, KALA JEREMIAH anatarajia kuachia ngoma yake nyingine … “Walewale”.  Katika WALE WALE, Kala amemshirikisha mwanadada mwenye sauti nzuri, NAY LEE …

Katika kuwapa burudani wapenzi wa nyimbo zake ikiwemo hii itayotoka ndani ya week moja, KALA amepanga kuachia kwa mpigo kazi zake hizo, yaani AUDIO Na VIDEO ndani ya siku moja..

“Tarehe 20 mwezi huu wa 11 mwaka huu wa 2013 jumatano ya wiki ijayo wimbo wangu mpya unaokwenda kwa jina la walewale niliomshirikisha Naylee unatoka rasmi audio na video kwa pamoja..Asanteni sana” , ameandika Kala Jeremiah kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram masaa machache yaliyopita

KALA JEREMIAH anaendelea kufanya vizuri na ngoma zake kama “KARIBU DAR” ambayo alimshirikisha mkali wa RnB, BEN POL, na pia “DEAR GOD” single ilyofanya vizuri zaidi na kumpelekea kutwaa tuzo ya KILI kama mwana-HIP HOP Bora kwa huu …

KALA amefanikiwa kupata shavu la kuwa balozi wa Pepsi ambalo linaendelea kumuingizia mkwanja mwingine ukiachana na shughuli za muziki za kila siku …

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post