ARSENAL WAAMUA KUFANYA KWELI, WATAKA KUMSAJILI CHICHARITO JANUARI NA NYOTA WENGINE KIBAO 'MAKINDA'

clip_image001[7]Anatakiwa: Arsenal imemuorodhesha mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez katika wachezaji inayotaka kuwasajili Januari

MTANDAO wa wasaka vipaji wa Arsenal umepiga hatua kubwa na sasa unataka kumsajili mshambuliaji asiyefurahia maisha Manchester United, Javier Hernandez 'Chicharito' katika dirisha dogo la usajili Januari.

The Gunners imejadili uhamisho wa kushitua wa nyota huyo wa Mexico, kutokana na kuwa na mshambuliaji mmoja tu, Olivier Giroud.

Arsene Wenger anafahamu mapungufu ya washambuliaji aliyonayo, Giroud akiwa mtu pekee aliyenaye katika safu hiyo.

clip_image001[9]Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez anabaki kuwa mchezaji aliye ndoto za Wenger kumsajili, lakini Hernandez yuko juu katika orodha ya wanaoweza kusajiliwa.

Arsenal itajaribu kusajili mshambuliaji mpya Januari, na kumtokea kwao Hernandez inaweza kuwa sahihi kutokana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutopewa nafasi kubwa ya kucheza Old Trafford.

clip_image001[5]Tegemeo pekee: Arsenal ina mapungufu ya washambuliaji, Olivier Giroud akiwa mtu pekee wa safu hiyo kikosini

Wenger - ambaye pia anammezea mate mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente anayemtaka kwa mkopo, anahofia Giroud anaweza kuumia na ndiyo maana anataka kusajili mshambuliaji mpya Januari.

Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi za Arsenal katika Ligi Kuu msimu huu pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hali inayozua hofu anaweza kuchoka au kuumia.

clip_image001Bado inamtolea macho: Wasaka vipaji wa Arsenal wanamfuatilia beki wa kulia wa Monaco, Fabinho

Wakati huo huo, Wasaka vipaji wa Gunners bado wanaendelea kumfuatilia beki wa kulia wa Monaco, Fabinho.

Mbrazil huyo anayecheza kwa mkopo kutoka Rio Ave, amevutia katika Ligue 1 msimu huu, na kiwango chake kimemkuna Msaka vipaji wa Arsenal aliye Ufaransa, Giles Grimandi. Wenger amewaambia wachunguzi wake kumtambulisha beki mpya wa kulia akihofia mustakabali wa muda mrefu wa Bacary Sagna katika klabu hiyo.

Mfaransa huyo hafiksihi mwaka katika Mkataba wake aliobakiza na bado anasuasua kusaini Mkataba mpya.

Makinda wenye vipaji wa Brazil, Boschilia na Nathan - ambao wamefunga mabao 11 baina yao katika Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17 Falme za Kiarabu (UAE) pia wameivutia The Gunners.

Msaka vipaji Mkuu, Steve Rowley amewatazama wawili hao katika michuano hiyo, na wasaka vipaji wataendelea kufuatilia maendeleo yao. Mshambuliaji wa Standard Liege, Michy Batshuayi, pia yupo kwenye rada za Arsenal.

Msaka vipa wa Ulaya, Ty Gooden amekuwa akimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ubelgiji, ambaye amefunga mabao 14 msimu huu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post