Unknown Unknown Author
Title: VIJUE VYUO 10 VILIVYOFUTWA NA SERIKALI, ANGALIA USIJE UKADANGANYIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta  vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NAC...
clip_image002
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta  vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NACTE)
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini  Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii  na kuongeza  kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa  kusajiliwa.
Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and  Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The  Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center,  vyote vya Dar es Salaam.
Vingine ni Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values  Training Institute na Information Technology Training Center  vya Dar es  Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha   Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa  mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo  urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa  mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea  kujaza fomu za mikopo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top