Mawaziri wa kigeni kutoka Afrika wamekutana mjini Addis Ababa Ethiopia kujadili uhusiano wa Afrika na Mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC.
Kabla ya kikao hicho cha faragha siku ya ijumaa, mwenyekiti wa zamu wa baraza la mawaziri wa umoja wa afrika ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia Tedros Adhanom aliishutumu ICC kwa kuwa na uonevu kwa nchi za Afrikaa.
"Badala ya kuhimiza haki na maridhiano na kuchangia kudumu kwa amani na utulivu barani afrika, hii mahakama ya ICC imebadilika kuwa chombo cha kisiasa kinacholenga Afrika na watu wake. Tunaona hilo sio sawa na kamwe halitakubalika"
Mkutano huu maalumu wa umoja wa Afrika unafanyika wakati kesi za rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto zinaendelea mjini The Hague. Viongozi hao wawili wanatuhumiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchanguzi wa mwaka 2007 zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 1200.
Uwezekano wa nchi za Afrika kujiondoa kwa pamoja kwenye mahakama ya ICC kumetokana na kuchanguliwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama Rais mapema mwaka huu na uamuzi wa bunge la Kenya mwezi Septemba wa kukatiza uhusiano wake na ICC.
Hata hivyo, haijajulikani kama nchi zote 34 wanachama wa ICC kutoka Afrika zitafikia uamuzi wa pamoja wa kujiondoa kutoka kwa mahakama hiyo ya ICC.
Baadhi ya nchi kama Ghana na Botswana tayari zimepinga hatua ya kujiondoa kutoka kwa ICC.
Lakini mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bi Dlamini-Zuma anasema umoja huo daima utajihusisha na maswala na matatizo ya kila nchi mwanachama.
"OAU ilipoanzishwa, sera yake ilikuwa ni kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ama mipangilio ya kimataifa, na hata baada ya kuunda AU, bado tunashikilia sera hiyo na ndio maana swala lolote linalohusu nchi ya Afrika ni jukumu la Umoja wa Afrika"
Hivi sasa kesi 20 kutoka Afrika zimewasilishwa katika mahakama ya ICC .
Jambo hili limezua maoni tofauti barani Afrika ikiwemo kujiondoa kutoka kwa mahakama hiyo. Viongozi wa nchi na serikali wa Afrika wanakutana leo jumamosi kukamilisha mjadala huu wa swalala ICC.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.