STERLING AITWA ENGLAND, RVP AWEKA REKODI HOLLAND!

clip_image001WINGA Chipukizi wa Liverpool, Raheem Sterling, ameitwa kwenye Mechi ya mwisho ya England ya Kombe la Dunia hapo Jumanne watakapocheza Uwanja wa Wembley na Poland ili kumbadili Majeruhi Tom Cleverley wa Manchester United na huko Holland, Straika wa Man United, Robin van Persie, Jana alifunga Hetriki wakati Holland ilipoichapa Hungary Bao 8-1 kwenye Mechi ya Kombe la Dunia na kuweka Rekodi ya yeye kuwa ndie Mfungaji Bora wa Nchi hiyo.clip_image001[7]KOCHA wa England Roy Hodgson amemchukua Winga wa Liverpool, Raheem Sterling, ili kumbadili Mchezaji wa Man United Tom Cleverley ambae ameumia.

Sterling, ambae hajaichezea England tangu Novemba, ameitwa ili kuziba pengo hilo kwa ajili ya Mechi ya mwisho ya Kundi H la Kombe la Dunia dhidi ya Poland ambayo ushindi kwa England utawapeleka Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Mechi hiyo na Poland itachezwa Jumanne Uwanja wa Wembley Jijini London.

Jana England iliwapoteza Wachezaji wawili, Tom Cleverley, na Kyle Walker ambae alipewa Kadi ya Njano kwenye Mechi ya Jana na Montenegro na hivyo kufungiwa Mechi moja.

Mwezi Novemba, Sterling, mwenye Miaka 18 na Mzaliwa wa Jamaica, aliichezea England kwa mara ya kwanza ilipocheza na Sweden.

RVP AWEKA REKODI HOLLAND!clip_image001[5]STRAIKA wa Manchester United Robin van Persie alifunga Hetitriki Holland ilipoichapa Hungary Bao 8-1 kwenye Mechi ya Kundi lao la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil Mwakani na kuweka Rekodi ya kuwa ndie Mfungaji Bora wa Nchi hiyo katika historia yao.

Bao hizo 3 zimemfanya ampiku Patrick Kluivert na sasa kuwa na Bao 41 katika Mechi 80.

Patrick Kluivert sasa ni mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya Holland chini ya Luis van Gaal.

SOURCE: SOKAINBONGO

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post