Facebook kuna vituko sana.Nilikuwa katika upekuzi wangu wa kawaida mtandaoni, nikaona si mbaya nikiingia facebook ili nione dunia inaendeleaje.
Ndani ya facebook kuna ma-group mengi ambayo nayapenda likiwepo hili la jamii forum halisi.Nilipolifungua, post ya juu kabisa ilikuwa ni FUMANIZI LA TUNDU LISU..
PICHA YA JUU NDO POST YENYEWE:
Post hiyo ilikuwa inasimulia umalaya wa Tundu Lissu na jinsi alivyochaniwa shati lake baada ya kufumaniwa na wananchi....
Niliduwaa kwa muda huku nikiwa siyaamini macho yangu...Baada ya kuingalia picha ilyopachikwa, niligundua kwamba huo ni uzushi kwa sababu picha naifahamu..
Ni picha iliyochukuliwa jijini Arusha wakati wa vurugu za CHADEMA na POLISI.
Baada ya post hiyo, kilichofuata kwa chini ni mvua ya matusi kwa aliyetoa habari hiyo.
SOURCE: MPEKUZIHURU.COM