Unknown Unknown Author
Title: POLISI WATUHUMIWA KUVUNJA WATU MIGUU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Askari polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabibo,  wanatuhumiwa kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono, wakazi wawili wa  eneo la Jitegem...
clip_image002
Askari polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabibo,  wanatuhumiwa kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono, wakazi wawili wa  eneo la Jitegemee.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 17 mwaka huu saa 5  usiku wakati wakazi hao, Maulid Yahaya na Willium Six, wakiwa wanakunywa  vinywaji kwenye duka lililopo eneo la Mabibo Mwisho.
Habari zilisema wakati watu hao wakijiburudisha,  alijitokeza mtu mmoja na kuaanza kuwafanyia fujo jambo lililosababisha  wote wawili kupelekwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mabibo.
Akizungumzia tukio hilo, Yahaya alisema wakati  tukio hilo likiendelea kufanyika, mtu huyo alichukua filimbi na kuanza  kuipiga ndipo walijitokeza watu na kuwapeleka kwenye kituo hicho.
Alisema walipofikishwa kituoni, ilitolewa amri na  polisi kuwa wapigwe kabla ya kuingizwa mahabusu ndipo alipojitokeza  askari polisi mwingine akiwa na mgambo ambao walianza kuwashambulia kwa  kutumia visu na virungu huku wakiwa wamefungwa pingu.
Alisema ilipofika saa 9 usiku walifuatwa na gari  la polisi na kuhamishiwa kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki ambako  walikaa mahabusu siku mbili bila ya kupelekwa hospitali.
Yahaya alisema wakiwa mahabusu waliwaomba askari  polisi, ili waweze kupelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa huduma  kutokana na majeraha waliokuwa wameyapata.
"Tunataka kujua sheria ipi inamruhusu askari polisi kumpiga raia akiwa mahabusu bila ya kusikiliza maelezo yake,” alisema Yahaya.
Kwa upande wake, Six alisema Oktoba 19 mwaka huu  saa 8 mchana waliruhusiwa kutoka kituoni baada kesi yao kufutwa na mtu  aliyewafanyia fujo wakati wanakunywa vinywaji.
Alisema baadaye walimfuata mmoja wa askari na  kumweleza kuwa walipigwa na askari wa Kituo Kidogo cha Polisi Mabibo  lakini alikataa kuchukua maelezo yao.
Six alisema walipelekwa Kituo cha Afya cha Sinza  ambako walipigwa picha ya X-ray na kugundulika kuwa mguu wake wa kushoto  umevunjika mara mbili huku Yahaya akiwa amevunjika mkono.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema hajapata taarifa na kwamba anafuatilia.
SOURCE: MWANANCHI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top