CHRIS BROWN AKAMATWA NA POLISI WASHINGTON DC

clip_image002Mwanamuziki wa Pop na R&B duniani, Chris Brown akamatwa leo asubuhi (0825 GMT) na kutiwa mbaroni na Polisi akiwa jijini Washington DC Marekani kwa kosa la kupigana na mtu ambaye haikujulikana ana uhusiano gani na msanii huyo.

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Christopher Hollosy na yeye pia alikamatwa na polisi na kupelekwa Hospital kwanza.

Chris Brown ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kazi za kusaidia jamii (community service) kutokana na kosa la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna … hivi karibuni na pia alikutwa na hatia ya kugonga mtu na kukimbia jijini Los Angeles, aliongezewa adhabu ya kusaidia kazi za kijamii kwa muda wa masaa 1000.

Ofisi ya wanasheria jijini Los Angeles, imemshtaki mwanamuziki huyo kwa kosa la kukwepa kutumikia adhabu yake ambayo Chris Brown anatakiwa kuitumikia baada ya kupewa ruhusa ya kutumikia adhabu hiyo nyumbani kwao Virginia.

SOURCE: GONGAMX.COM

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post