BPL::TETESI ZA USAJILI JANUARI: KAGAWA KURUDI DORTMUND, LLORENTE KUTUA ARSENAL

clip_image002ZIPO taarifa nzito kuwa Kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp anawania kumsaini tena Kiungo kutoka Japan anaechezea Manchester United, Shinji Kagawa, na huko Arsenal zimeibuka stori kuwa Mwezi Januari watamsaini Straika wa Juventus Fernando Llorente.

KAGAWA KURUDI DORTMUND?

SHINJI_KAGAWAKOCHA wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp anawania kumsaini tena Shinji Kagawa kwa kubadilishana na Beki Neven Subotic.

Kagawa, Mchezaji wa Kimataifa wa Japan, amekuwa hana namba ya kudumu tangu ahamie Man United kutoka Dortmund Msimu uliopita chini ya Meneja Sir Alex Ferguson na hata Msimu huu chini ya Meneja mpya wa Man United, David Moyes, Mchezaji huyo amekuwa hapangwi.

Hivi karibuni, Kagawa alikiri inabidi afanye bidii zaidi ikiwa atataka kupata namba Man United na pia aliweka wazi kuwa huenda akarudi Dortmund.

Kocha Jurgen Klopp Siku zote amekuwa akimsifia Kagawa na aliweka bayana atamkaribisha tena Kiungo huyo.

Ripoti zinadai David Moyes yuko tayari kumruhusu Kiungo huyo kurudi tena huko Dortmund ikiwa tu Klabu hiyo ya Bundesliga itawapa Sentahafu wao kutoka Serbia, Neven Subotic, mwenye Miaka 24.

Hata hivyo Dili hii ya kubadilisha Wachezaji inatarajiwa kuwa ngumu kukamilika.

LLORENTE KUTUA ARSENAL JANUARI?clip_image001[9]Arsenal wameripotiwa kuwa Mwezi Januari wakati Dirisha La Uhamisho litakapofunguka watatua huko Juventus kumchukua Straika wa Klabu hiyo ya Italy, Fernando Llorente.

Arsenal wana upungufu kwenye Safu ya Mastraika na inadaiwa Meneja wao Arsene Wenger yuko tayari kumwaga Fedha nyingi kumnasa Fowadi huyo wa Spain.clip_image001

Hivi sasa tegemezi kubwa la Arsenal ni Olivier Giroud baada ya Lukas Podolski na Theo Walcott kuwa nje kwa maumivu.

Llorente ameshindwa kupata namba ya kudumu huko Juventus tangu ahamie hapo kutoka Atletico Bilbao mwanzoni mwa Msimu huku Mabingwa hao wa Italy wakiwachezesha kina Carlos Tevez katika Mechi nyingi Msimu huu.

RATIBA:

BPL: LIGI KUU ENGLAND

[Saa za Bongo]

MECHI ZIJAZO:

Jumamosi 19 Oktoba

14:45 Newcastle United v Liverpool

17:00 Arsenal v Norwich City

17:00 Chelsea v Cardiff City

17:00 Everton v Hull City

17:00 Manchester United v Southampton

17:00 Stoke City v West Bromwich Albion

17:00 Swansea City v Sunderland

19:30 West Ham United v Manchester City

Jumapili 20 Oktoba

18:00 Aston Villa v Tottenham Hotspur

Jumatatu 21 Oktoba

22:00 Crystal Palace v Fulham

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post