BOB JUNIOR ATANGAZA RASMI KUWA YEYE NI SINGLE BOY, NDOA YAVUNJIKA SOMA MKASA

clip_image003Msanii Bob Junior amefunguka leo kupitia sammisago.com kuwa yuko single baada ya ndoa yake kuvunjika mwezi moja uliopita. Wasanii wengi huwa wanapata wakati mgumu wanapo funga ndo kwa sababu ya umaarufu na ratiba za maisha yao kabla ya kufunga ndoa.

Bob Junior leo mchana ametambulisha wimbo wake mpya na kutoa taarifa kwa mabinti wote kuwa kwa sasa Bob Junior ni single boy kumanisha kuwa ameachana na mke wake mwezi moja uliopita.

Kuogopa kuweka mambo ya familia waze Bob Junior hajasema haswa Sababu ya kuachana na mke wake ila ameniambia kilicho changia ndoa yake kuvunjika ni Wivu wa mke wake.

Bob junior ameniambia kuwa wivu ni moja ya sababu zilizofanya ndoa yake kuvunjika na kwamba  alikuwa na wakati mgumu sana kumuonyesha mke wake kuwa yeye ni muaminifu kutokana na kuwa star na kupendwa na mashabiki wa Kike.

Fahamu kuwa ndoa ya Bob Junior Imedumu kwa Mwaka Moja Na miezi 2 tu.

Ladies Bob Junior Is Available. lol

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post