BAADA YA KUZUNGUSHWA NA DAWASCO WANANCHI WA MWENGE NYUMA YA MAGHROFA YA JWTZ WAAMUA KUJITOA MUHANGA NA KUSHIKA KINYESI KUZIBUA CHEMBA ZA MAJI TAKA

clip_image002Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate  kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita

Wananchi mtaa wa mwenge waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa ilyokuwa sugu na hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka kwa chemba zinazo pitisha maji machafu maarufu kama (majitaka

Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa ambalo ni mtaa wa(kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za maji taka na kuwa na harufu mbaya hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi.

Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu mbalimbali.

Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya mara kadhaa bila mafanikio

Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi

mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji (DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja ili kuweka mazingira mazuri/safi.

Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibuaHali ni Tete eneo Hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo  maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.Ilikuwa ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia wenyewe, hatimaye  walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.Zoezi sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3  ambapo sasa  walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa  imejaa matakataka ya kutosha pamoja na Mchanga .

Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO wanakuja.Wakiwa wamefika  kabisa na kujionea Adha ya kukanyaga maji Taka ...... huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua ChembaWafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua  chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe  na magonjwa , Kero ya maji mtaani na Harufu mbayaWakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo...Moja ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kufanikiwa  kutoa maji taka hayo  yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCOWafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapiteHii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo la tukioMaji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwaHizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ...

PICHA NA DAR ES SALAAM YETU

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post