Zaidi ya magari ya mizigo 400 yaliyokuwa yamekwama katika eneo la Rusumo mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda baada ya serikali ya Rwanda kupandisha kodi ya kutoka dola 152 hadi dola 500 kwa kila gari moja la mizigo na kusababisha msongamano mkubwa mpakani
Hapo yameanza kupita kufuatia tozo hiyo mpya kusitishwa ambapo magari mengi yanapita Rwanda kwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo .
Wakizungumza na itv kabla ya kuruhusiwa baadhi ya madereva wa magari ya mizigo wameiomba serikali ya Rwanda kufanya makubaliano na nchi wanachama wa afrika mashariki kwa kuwa na lugha moja ya kodi na kwamba marumbano yaliyopo kati ya rais wa nchi ya Rwanda na Tanzania na kwamba rais wa Rwanda amepandisha gharama bila taarifa kwa wasafirishaji hali inayosababisha usumbufu kwa madereva.
Kwa upande wake mmoja wa watendaji wa serikali wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) aliopo katika eneo la mpaka wa tanzania na nchi ya Rwanda Bw. Nasoro Ibrahimu amekili kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari ya mizigo katika eneo la tanzania baada ya kuzuiliwa kuingia katika nchi ya Rwanda hali iliyosababisha kufunga barabara ya rusumo ngara isipitike
source: ITV WEBSITE
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.