WAZEE wa Yanga waliokasirika na ‘kuipiga laana’ timu baada ya kutofautiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga ikapigwa 5-0 na Simba SC mwaka juzi, wameingia katika mgogoro mwingine na uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
Wazee hao chini ya kinara wao, Ibrahim Ally Akilimali wanaingia katika mtafaruku na uongozi wa Manji, kiasi cha mwezi mmoja na ushei kabla ya mchezo mwingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Oktoba 20, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya kutoka Kenya.
Katibu Mkuu mpya wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.