Unknown Unknown Author
Title: YANGA YATOA UFAFANUZI JUU YA TAARIFA YA KATIBU MKUU MKENYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya habari zilizo...
clip_image001Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya habari zilizokuwa zimeenea kuhusiana na taarifa za mabadiliko ya kaimu katibu mkuu Lawrence Mwalusako kuondolewa kwenye nafasi yake na kuchukukuliwa na mtu mwingine.
Akiongea na waandishi wa habari Sanga amesema taarifa hizo hazina ukweli kwamba tayari kuna mtu anachukua nafasi ya Mwalusako, bali kilichotokea ni kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri katika suala hilo kati ya viongozi na wazee.
Kilichopo ni kwamba uongozi wa klabu ya Young Africans upo katika mchakato wa kuhakikisha unajaza nafasi zilizopo wazi za mkurugenzi wa ufundi, mkurugenzi wa masoko, mkurugenzi wa fedha na zoezi hilo linaendeshwa na kampuni moja ambayo waliipa nafasi ya kuendesha zoezi hilo.
Zoezi likiwa ndani ya mchakato mmoja wa waombaji wa nafasi hizo Patrick Naggi aliwasili makao makuu ya klabu ya Yanga kwa lengo la kutaka kujua mazingira ya ufanyaji kazi yakoje na kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na klabu ndipo kulipotokea kutokuelewana na baadhi ya wanachama wakiwemo wazee waliokuwepo eneo la klabu.
Kwa maana hiyo napenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote katika nafasi hizo, isipokuwa ni muombaji aliwahi kufika makao makuu kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.
Lawrence Mwalusako anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi katika idara mbalimbali.
Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani wa kimatifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top