Unknown Unknown Author
Title: NANI KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA TUSKER PROJECT FAME 6!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Tusker Project Fame, shoo halisi ya muziki ambayo inapagawisha watazamaji na mashabiki kwa ujumla Mashariki mwa Afrika. Sasa imerudi tena ka...

clip_image001Tusker Project Fame, shoo halisi ya muziki ambayo inapagawisha watazamaji na mashabiki kwa ujumla Mashariki mwa Afrika. Sasa imerudi tena katika msimu wa 6 ambapo msimu huu itakua ya aina yake kwa ukubwa na nzuri zaidi kulinganisha na misimu iliyopita.

Miliki jukwaa! Tusker inawaalika wale wote wenye vipaji vya kuimba kufika katika usaili tarehe 7 na 8 Septemba, 2013 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo washiriki wa Tanzania watapata nafasi ya kuingia katika jumba la Tusker project Fame na kushindanishwa jukwaani na vinara kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

Zawadi ni nono msimu huu, na mshindi wa Tusker project Fame atajinyakulia kitita cha Sh. 100,000,000 za kitanzania na kupata mkataba mnono wa mwaka wa  kurekodi wenye thamani ya Sh. 200,000,000 za kitanzania. Ni imani yetu kwamba fedha zitabebwa na mtanzania kwani vipaji tunavyo vya kutosha kikubwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika usaili huu.

Katika msimu huu mpya watu wengi zaidi watahusika katika shughuli mbalimbali uwanjani hata kumiliki jukwaa. Kujiunga na hayo yote shiriki katika promosheni zinazoendelea katika bar mbalimbali na upate ofa za Tusker.

KUHUSU USAILI

Tusker Project Fame kupitia bia yake ya Tusker Lager inatafuta vijana wenye vipaji vya kuimba nawenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika soko la muziki pia wenye utaalamu wa hali ya juu katika kuimba na kutumia vifaa vya muziki ipasavyo. Wapenzi wote wa muziki ambao wana weledi wa kutosha kuiwakilisha Tanzania na kuonesha kuwa wanaweza kufanikiwa na kujulikana kama nyota katika muziki wanakaribishwa sana.

Wale wenye vipaji vya muziki wanaweza kujaribu bahati kwa kujitokeza katika usahili wa Tusker project fame. Siku mbili za usaili kwa ajili ya kusaka mastaa wa msimu wa 6 wa Tusker Project fame utakaofanyika jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo:

Tarehe 7 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi

Tarehe 8 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi

Washiriki waje wakiwa tayari kuwakabili majaji wetu ambao wataangalia kipaji, kujiamini na kubwa zaidi wataangalia washiriki ambao wateweza kufundishika na wale watakaoibuka vinara kwa wenzie.

Usahili wa Tusker Project Fame ni kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 18.

ITAONYESHWA

Msimu wa sita wa Tusker Project Fame inarushwa hewani kupitia katika vituo vya televisheni vya EATV saa 2 usiku na ITV saa 4 usiku.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top