Unknown Unknown Author
Title: WILAYA YA KILWA YAKUSANYA ZAIDI YA TSH MILIONI 600 KATIKA KIPINDI CHA MWAKA KUPITIA MISITU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Zaidi ya shilingi milioni 600 zimekusanywa na wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi ktk kipindi cha mwaka 2013/2014 baada ya kuuza kawa njia ya mnada...

DSC06823Zaidi ya shilingi milioni 600 zimekusanywa na wilaya ya Kilwa Mkoani
Lindi ktk kipindi cha mwaka 2013/2014 baada ya kuuza kawa njia ya
mnada mazao mbali mbali ya misitu ya hifadhi yaliyokamatwa ndani ya wilaya hiyo.

Akizungumza na blog hii wilayani humo, Meneja wa wakala wa misitu ktk wilaya hiyo ya Kilwa, Kashenge Salhina ameyataja mazao
yaliyokamatwa na kuuzwa kwa njia ya mnada, kuwa ni zaidi ya mbao
2,670, magogo 803, zaidi ya magunia 1,000 ya mkaa pamoja na tozo
kutokana na kuzidisha mzigo kulingana na leseni ya mfanyabiashara
husika.
DSC06832Aidha alibainisha kuwa kiasi kikubwa cha mazao hayo ya misitu
yaliyovunwa yamekuwa yakisafirishwa nje ya wilaya hiyo kupitia njia za panya zikiwemo bandari bubu zilizotapakaa ktk maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo ya Kilwa kwa kutumia usafiri wa majahazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya uvunaji misitu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega amesema pamoja na kwamba wilaya yake imefanikiwa kuwadhibiti wavunaji haramu wa mazao ya misitu, bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuibuka kwa wakulima wa zao la ufuta wanaovamia misitu iliyotengwa kwa ajili ya hifadhi.DSC_0330Pamoja na mafanikio hayo Mtendaji wa kijiji cha Kiwawa na Mwenyekiti walieleza masikitiko yao kufuatia kijiji kutopata mapato ya msitu huo licha kuwa ndio watunzaji na wakamataji wa mazao hayo huku wakitishiwa maisha yaoDSC06825Vijiji vya Kiwawa, Kinjumbi,na Somanga Vimeshamiri kwa uharibifu
mkubwa wa misitu unaofanywa na baadhi ya wananchi kwa kukata miti kwa ajili ya mbao, magogo,mkaa na kilimo cha kuhamahama kila mwaka na kusafirisha katika Bandari Bubu

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top