Unknown Unknown Author
Title: USAHILI WA MISS UNIVERSE TANZANIA KUFANYIKA NYUMBANI LOUNGE KESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications inakamilisha jumamosi hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam. Timu ...
clip_image001Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications inakamilisha jumamosi hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam.
Timu ya Miss Universe Tanzania ilifanya mchakato wa usaili na picha (scouting) katika mikoa 8 ambayo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Miss Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake mwezi Septemba taehe 27 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert street jijini Dar es Salaam.
Mashindano ya mwaka huu umepata wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mohamed Enterprises na Fastjet. Wadhamini wengine watajulikana ndani ya siku chache. Wadhaimini wote watatambullishwa wiki ijayo.
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010.
Baadae taji lilichukuliwa na Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic
SOURCE: MTAA KWA MTAA BLOG





About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top