Unknown Unknown Author
Title: MCHEKI WAYNE ROONEY AKILA BATA WAKATI WENZIE WAKIJIANDAA NA MECHI MUHIMU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Striker wa Manchester United na Timu ya taifa ya England Wayne Rooney amekuwa akijipumzisha na familia yake huko Ureno ambako anarudi kweny...

clip_image002Striker wa Manchester United na Timu ya taifa ya England Wayne Rooney amekuwa akijipumzisha na familia yake huko Ureno ambako anarudi kwenye hali ya uzima baada ya jeraha baya alilolipata kichwani wakati wa mazoezi na klabu yake baada ya kupigwa ‘buti’ na beki Phil Jones.Rooney akiwa na Mkewe Coleen na mtoto wao Kai.Rooney akiwa na Mkewe Coleen na mtoto wao Kai.

Kidonda chenye shimo lililochimbika kwa karibu nchi mbili hakijamzuia Rooney kwenda kuweka kambi ya muda ndani ya hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Conrad ambayo iko kwenye viunga vya Mji wa Algarve vya Quinta De Logo ambapo ameambatana na mkewe Coleen McLoughin na mtoto wake wa kwanza Kai.Hoteli aliyofikia Rooney huko Ureno.Hoteli aliyofikia Rooney huko Ureno.

Wakati Rooney akiuguza kidonda chake kwa bata la nguvu wenzie wa timu ya taifa ya England wako nchini Ukraine ambako wanajiandaa kwa mchezo wa kufuzu kombe la dunia kwa kanda ya UEFA dhidi ya Ukraine huko Kiev.Wachezaji wa England wakikatiza kwenye mitaa ya Jiji la Kiev ambako watakuwa na mechi dhidi ya timu ya taifa ya Ukraine.Wachezaji wa England wakikatiza kwenye mitaa ya Jiji la Kiev ambako watakuwa na mechi dhidi ya timu ya taifa ya Ukraine.

Bado haijafahamika lini Rooney atarudi uwanjani baada yacha za kidonda chake kuonyesha kuwa ni kidonda kikubwa kuliko ilivyodhaniwa awali .Kidonda kilichopo usoni kwa Wayne Rooney alichopata mazoezini akiwa na Man United.Kidonda kilichopo usoni kwa Wayne Rooney alichopata mazoezini akiwa na Man United.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top