Unknown Unknown Author
Title: VIDEO: DAKTARI AMTANDIKA NGUMI MGONJWA BAADA YA KUPISHANA KAULI....
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Daktari mmoja nchini Urusi, Andrey Votyakov (bingwa katika fani ya usingizi) mapema mwezi uliopita alitimuliwa kazi baada ya video ya chumba...

clip_image001Daktari mmoja nchini Urusi, Andrey Votyakov (bingwa katika fani ya usingizi) mapema mwezi uliopita alitimuliwa kazi baada ya video ya chumba cha upasuaji inayorekodi matukio (surveillance camera) kuoneshwa hadharani ambapo daktari huyo alionekana akilumbana na mgonjwa aliyefungwa kitandani na baadaye kumshushia makonde usoni na kifuani, upande wa kushoto.

Mgonjwa huyo aliyekuwa katika kitendo cha magonjwa ya moyo, alikuwa wa umri wa makamo (miaka 45) na alifariki muda mfupi baadaye.
Tukio hilo lilitoea mwezi Februari mwaka huu lakini liligundulika mwezi Julai.
Daktari huyo ambaye hakuwa na rekodi yoyote mbaya kazini, alijitetea kuwa alipandwa na jazba baada ya mgonjwa kumsemea maneno yaliyomuudhi na kujikuta amempiga.
Vile vile alisema uchovu uliotokana na kufanya kazi mfululizo kwa saa 24, ulichangia kushindwa kwake kufanya maamuzi yenye busara.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top