Unknown Unknown Author
Title: UAMSHO KUMFIKISHA SHEIKH SORAGA MAHAKAMANI KWA SUALA LA TINDIKALI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) inakusudia kumfikisha katika vyombo vya sheria Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh...

clip_image001Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) inakusudia kumfikisha katika vyombo vya sheria Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, kutokana na kuishutumu Jumuiya hiyo kuhusika na tukio la kuwamwagia tindikali mabinti wawili raia wa Uingereza.

Amir Haji, mlezi wa Jumuiya hiyo, alisema wamesikitishwa na taarifa zilizotolewa katika magazeti mbali mbali ya hapa nchini likiwemo Tanzania Daima, Mtanzania, Zanzibar Leo na Uhuru yaliyomnukuu Sheikh Soraga huyo kuihusisha Uamsho kuhusika na tukio hilo.

“Uislamu unakataza kufanya mambo maovu kwa kujidhuru mwenyewe au mtu mwengine aliye Muislamu na asiyekuwa Muislamu”, alisema Amir Haji na kuongeza kuwa mara nyingi Jumuiya hiyo imekuwa ikipakwa matope kuhusishwa na uovu kama huo ilhali haina malengo hayo.

“Cha kusikitisha zaidi ni kiongozi Muislamu kusema maneno kama hayo ya kutupaka matope. Shutuma hizi zimezidi mipaka na ndugu yetu Sheikh Soraga amelipalia makaa. Kila siku tunapakwa matope. Lakini tunamuomba kama hana la kusema basi anyamaze na kama ana ushahidi basi autoe katika vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake“, alisema Amir Haji, ambaye pia amemtaka Katibu huyo wa Mufti  kuwaomba radhi Waislamu na jumuiya hiyo.

Kwa upande wake Katibu wa Uamsho, Said Hamad, ameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kina wa kubaini wahalifu waliotenda unyama wa kuwamwagia tindikali wasichana wawili wa Kiingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa 18, na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo kuendelea hapa nchini.
Katibu huyo wa Uamsho aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kina kwa jeshi la Polisi nchini ili kufanikisha uchunguzi juu ya tukio hilo.

SOURCE:  ZANZIBARDAIMA.net

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top