THEA: ‘KIYAMA’ CHA WASANII MAMISI KIMETIMIA

clip_image002

Na Gladness Mallya
BAADA ya wasanii waliotoka kwenye mashindano ya u-miss kuvuma sana na kupotea ghafla, msanii mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka na kudai utabiri wake umetimia.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Thea alisema miaka kadhaa iliyopita alitabiri kuwa wasanii waliokuwa wanavuma sana ambao walitokea kwenye mashindano ya u-miss, hawatadumu kwenye uigizaji hivyo utabiri wake umetimia kwani sasa hivi, hawavumi tena.
“Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya u-miss wengi hawasikiki tena, wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, tulisota sana kwenye vikundi,” alisema Thea.

CREDIT TI GPL

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post