Unknown Unknown Author
Title: SIMULIZI: SEHEMU YA KUMI NA TATU NA YA MWISHO YA “PLAY BOY”
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Simulizi: Play Boy (Jeff wakujidai) Sehemu: 13 (Mwisho kabisa) Mtunzi: Andrew Carlos Simu: 0713 133 633 Ilipoishia jana.. "...Sammy, e...

clip_image003Simulizi: Play Boy (Jeff wakujidai)
Sehemu: 13 (Mwisho kabisa)
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: 0713 133 633

Ilipoishia jana..
"...Sammy, embu sogeza sikio nikunong'oneze kitu.."
Alisogeza masikio yake na hapo hapo ikawa mwanya wa kuanza kuingiza ulimi wangu kwenye masikio yake, Ghafla akanitoa kwa nguvu nakuanza kulalamika huku akiniangalia kwa sauti ya kimahaba..
"..Jeff sipendi na sipendi mwanaume yeyote aniingizie ulimi wake masikioni mwangu.."
Songa nayo sasa…
"..ooh samahani sana.."Nilimjibu kwa sauti ya upole
nakumfanya tukae naye karibu kwenye kochi.
"ah liwalo na liwe bwana.."
Nilijipa moyo nakuuchukuwa mkono wangu kwa taaratibu nikaanza kumpapasa mapajani mwake huku nikikaribia maeneo yetu yale..
"..Jeff stooop.. Stop pliiz.." Sammy aliongea kwa sauti ya chinichini na ya kimahaba huku  akionesha kashalainika.
Nilijifanya sijaisikia sauti yake, nikazidisha kumpampasa na sasa hivi nilikuwa kiefuani mwake huku nikichezea chuchu zake..
"..Jeff najuta kukuleta hapa kwangu.." Aliendelea kusema huku anahema juu juu.
Niliiuchukuwa mdomo wangu nakuushikanisha na mdomo wake
kisha tukabadilishana mate kwa kutumia ndimi zetu,
Mapenzi yalikolea mpaka mwenyewe akanivulia blauzi yake na kisha mini nakubakiwa na chu** tu..
Hapo kazi yote ilibaki kwangu kwani nilimlegeza mpaka akalegea vya kutosha, sauti yake ilikatika ghafla kabla sijaanza kufanya chochote, mwanzo nikahisi labda huenda utamu umemkolea lakini haikuwa hivyo
kwani nilipomshika mapigo ya moyo alikuwa ahemi kabisaa..
Ghafla nikawa kama mtu aliyechanganyikiwa, nilijaribu kumuamsha tena kwa mara ya pili lakini bado hali yake ilikuwa tete..
"..ina maana ndio kafa au..?"
Ni kati ya swali niliokuwa najiuliza bila kupata jibu..
*****************
Mpaka giza linaingia bado Sammy alikuwa hajaamka, nikiwa bado naki boxer changu huku mwili wangu ukiwa kama umepigwa ganzi, simu yangu nilikuwa nimeizima na sikutaka mawasiliano yoyote,
Japo nilianza kuisikia njaa lakini hamu ya kula sikuwa nayo kabisa.
Kila baada ya dakika 5 hadi kumi nilikuwa namshtua lakini hali yake ikabaki vile vile.
Akili niliyokuja kuipata nikumbeba pale sebuleni mpaka chumbani kwake nikamlaza kitandani kwake nakumfunika na shuka kidogo kwa nia ya kumtoroka, baada ya hapo nikanyata nakutoka chumbani lakini kabla sijafika sebuleni nikajikuta nimesahau simu yangu nilipomlaza tu pale kitandani.
Nikairudia haraka haraka nakuichukuwa kisha nikamfunua lile shuka nakumuangalia kwa mara ya mwisho.
"..bwana ametoa na bwana ametwaa.. Apumzike kwa amani.."
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini kisha nikambusu shavuni mwake Sammy huku mchozi ukinilengalenga..
Taaratibu nikaliona jasho linamvuja Sammy likitokea kichwani likipitia shingoni mwake..
Nilipigwa na butwaa kama dakika 5 nzima, nikachukuwa mkono wangu nakugusa mapigo yake ya moyo kwa mara nyingine tena..
"...oh yees!! Yee!!"
Furaha ya ajabu ikanitawala huku mwili wangu ukisisimka nakusababisha kama kizungu zungu kwa kushuhudia mapigo ya moyo ya Sammy yakidunda..
Nilimtingisha kwa nia yakumuamsha na hatimaye akafumbua macho nakunifanya machozi ya furaha yachukuwe nafasi yake..
"..Jeff.. Jeff mpenzi.." Aliachama mdomo nakuniita..
"..niambie mpenzi wangu Sammy.."
"..do you know how much I love you..? (unajua ni jinsi gani nakupenda..)
"..yeah, najua Sammy.." Mud wote huo sammy alikuwa akiongea huku anatia huruma nakunifanya nimjibu huku machozi yakinilenga lenga.
"..Jeff najua unatembea na rafiki yangu Irene, pia unamchumba wako Jacky, lakini na mimi nipo katika hifadhi hiyo hiyo.."
Nilihisi kama Sammy kachanganyikiwa fulani kwa kuongea maneno yale..
"..sawa nimekuelewa Sammy embu tuongelee mambo mengine.."
Nilimkatisha maneno yake aliyokuwa anaongea.
Alichokifanya alichukuwa mikono yake nakulivuta shuka kisha akalitua nakubakiwa uchi kabisa kisha akainuka nakunisogelea huku akiitumia ile mikono yake kuipitisha shingoni mwangu nakuanza kunipa denda..
Mwili wake bado ulikuwa wamoto sana. Na muda wote sikutaka kumuuliza chochote juu ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ule..
Nilimpindua nakumrushia kitandani mwake kisha kilichofuata ni kumpa anavyotaka tena kwa kila staili huku tukimaliza akibaki hoi anahema juu juu..
Tulipomaliza tulijikuta kwa wote usingizi ukitunyemelea hivyo tukalala mpaka asubuhi..
Nilikuja kushtuka asubuhi asubuhi nikaichukuwa simu yangu nakuiwasha,
Meseji ziliingia mfululizo zote zilikuwa zinatoka kwa Irene, nikafungua nakuzisoma haraka haraka..
'..UKO WAPI? JACKY NIMEMPA NAULI AMESEMA ANARUDI DAR..
ANASHUKURU KWA ULIVYOMZIMIA SIMU NAKUMTOROKA...
Akili yote ilinichemka huku kijasho chembamba kikiendelea kutoka ndani ya mwili wangu,
Niliiangalie ile meseji mara mbili mbili huku nikiwa sijiamini kabisa kama kweli imetokea kwa Irene au!
Niliipiga ile namba,
"..hallow Irene.."
"..Jeff uko wapi sa hivi toka jana..?"
"..samahanini kwa kutokuwaambia jana, nilipitiwa nikaenda 'club' lakini sasa hivi nipo njiani nakuja huko.."
"..kama unakuja wewe njoo tu, lakini tambua kuwa mchumba wako Jacky hayupo tena, nimeshampa nauli, na hivi ninavyoongea anaweza akawa ameshafika 'Chalinze' au Kibaha.."
"..unasemaje Irene..?"
Niliona kama ananidanganya, sikutaka kabisa kupoteza muda.
Nilivaa nguo zangu huku Sammy akiendelea kunitolea macho japokuwa alikuwa kachoka sana kwa shughuli tuliokuwa tunaifanya hapa kitandani.
Niliangalia muda ilikuwa tayari alfajiri kwenye saa kumi na moja.
"..hapa daladala lazima nitazipata tu.."
Nilijisemea peke yangu kwa sauti ya chini huku nikitoka chumbani nakuelekea sebuleni huku Sammy nikimwacha peke yake kitandani..
Nilipofika sebuleni napo nikakuta mlango umefungwa kwa ufunguo na ufunguo hamna, hivyo ikanibidi nirudi tena mpaka chumbani kumuuliza Sammy..
"...Sammy? Sammy pliz ufunguo wa sebuleni upo wapi..?"
"..angalia kwenye droo pale sebuleni.."
Sammy alichoka sana kwani hata kunyanyuka alishindwa.
Nikarudi tena sebuleni nakuuchukuwa huo ufunguo lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na hela kama shilingi elfu ishirini,Nikaichukuwa nakutoka mpaka nje huku nikielekea barabarani.
Ndani ya muda mfupi tayari nilikuwa ndani ya daladala huku mwili wote ukinitetemeka na hiyo yote nikumfikiria Jacky wangu.
"..sijui atakwenda kuwaambia kina Helleiner nilipo, maskini nimekwisha Jeff mimi nimekwisha.."
Nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani hata nilipofika stendi, nilikimbia mpaka maghorofani alipokuwa anaishi Irene.
Majasho yalinitoka sana, niligonga mlango kwa nguvu zote, Irene akafungua.
"..enhe mzee wa 'Club' bila kuaga karibu.."
Irene aliongea kiutani huku akiniangalia kwa jicho la kunitega.
"..niambie, Jacky wangu kweli hayupo..?"
"..nikwambie mara ngapi Jeff..? Hayupo enh..? Na ulipokuwa wote tunakujua na wala hatukutaka kukufuata.."
"..nilikuwa club kweli.."
"..ndio hapo ufafanue vizuri club ipi, au chumbani kwa Sammy kuna club..?"
Moyo ulinipasuka ghafla kwa mshangao huku nikiendelea kumtolea macho Irene..
"..hivi Jeff unajua kuwa Sammy anaundungu na Helleiner..?"
"..Helleiner..? Helleiner gani huyo..?"
"..unajifanya humjui eh, sasa hapa ulipo angalia kwa dirishani mapolisi hao wanakuja, na Jacky amekwenda kumchukuwa Helleiner huyo unayesema humjui.. Manake umeua huko ulipotoka unajifanya hujui enh..?"
Nilianza kuhisi mkojo unanitiririka ndani ya suruali yangu huku mishipa ikinitawala kwenye paji langu la uso ikiambatana na kajasho chembamba ambacho kalikuwa kakinitiririka shingoni kupitia makwapani mpaka kifuani kwangu..
"..Irene mie sijauwa mbona..? na Jacky ni mchumba wangu na hata wazazi wake wanajua, hawezi kufanya hivyo unavyoniambia.."
Nilijitahidi kujitetea huku nikijikaza nisionekane kweli nimeshawahi kuua, lakini Irene alionekana kucheka tu kila nilipojitetea.
Mara hodi ikapigwa pale kwa Irene, mapigo ya moyo ndo yakazidi kwenda kasi kabisa.
"..nimekwisha Jeff mie, nimekwisha..?"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikikata kabisa hamu ya kuendelea kuishi.
Irene alienda hadi mlangoni kufungua mlango nakuniacha nikiendelea kutetemeka mwili huku meno yakichukua nafasi yake kwa kuumana mithili ya mtu aliyemwagiwa maji ya barafu.
"..karibu, nikusaidie nini.?"
Ilikuwa ni sauti ya Irene. akiongea na huyo mtu ambaye hata sikumfahamu wala kumuona kwakuwa walikuwa wakiongea nje na mimi nipo kwa ndani.
"..Nauza, matunda na mboga za majani dada.."
Nilishusha pumzi chini baada ya kugundua kuwa hakuwa mtu mwenye kuniletea madhara bali ni muuza mboga na matunda tu.
Nilichokifanya nilikimbia mpaka chumbani kwa Irene na breki ya kwanza nikuchukuwa kipochi chake anachowekeaga pesa kisha nikafungua mlango wa jikoni nakutoroka zangu huku akili ikiwa ni moja tu ya kumpata mchumba wangu Jacky..
Ilinichukuwa kama dakika ishirini mpaka stendi ya mabasi yaendayo mkoani 'msamvu'.
Nilikata tiketi ya kuelekea Dar ile naingia tu kwenye basi nikashangaa nashikwa begani, mapigo ya moyo yakanibadilika ghafla lakini sikuonesha kukata tamaa kwani nilijigeuza taratibu huku nikiyakaza macho yangu.
"..unasemaje..?"
Maskini kumbe alikuwa ni mchumba wangu Jacky, alikuwa kavimba uso kweli nadhani ilitokana nakulia sana.
"..Jacky, unafanyaje hapa..?"
"..ni bora hata nimekuona, hapa nilipo nimechanganyikiwa Jeff, na hii yote kwa sababu yako, nilikuwa nirudi Dar kwetu nahapa unaponiona nimepoteza nauli sina hata senti tano na hii yote kutokana nakuchanganyikiwa.."
Taaratibu machozi yangu yalianza kunitoka yalioambatana na huzuni.
Nilitoa hela nyingine nakumkatia tiketi kisha tukaingia ndani ya gari tukisubiri gari ijaze ili tuondoke.
Tukiwa bado ndani ya gari huku Jacky wangu akinipa story kuhusiana na Irene,mara tukamuona huyo huyo Irene akiongozana na wavulana kama watatu hivi huku akija mpaka kwenye basi tulilokuwa tumepanda mie na Jacky wangu.
"..Jacky? Jacky wangu tumekwisha? tumekwisha Jacky? embu muangalie Irene huyo hapo kwa nje anakuja.."
Pale pale Jacky wangu akadondoka nakupoteza fahamu nakuniacha mwili umelegea, nilitamani nimbebe nakukimbia naye lakini ikawa ndo nimeshachelewa tena, hivyo Irene aliingia ndani ya basi na wale vijana wakanifunga pingu kisha wakamfunga pingu na Jacky wangu japo kuwa alikuwa ameshapoteza fahamu..
**************************
"... Jeff? we Jeff? embu hamka uko usingizi gani mpaka sasa saa tano za asubuhi..?"
"...aaah Mama..? umenikatisha ndoto niliokuwa naota bwana..?"
"..Jeff mwanangu lini utakuwa wewe? yani ndio kwanza unamiaka 16 embu nenda huko ukajiandae uende kanisani hujui kama leo jumapili.."
Nilijichekea peke yangu kwa ndoto ile nilioiota kwa usiku, kwani ilikuwa ndefu na iliyonikutanisha na wasichana wengi.
"..Mungu ninusuru na ndoto mbaya hizi..?"
Nilipiga goti nikasali kisha nikaenda kujiandaa kwa kuelekea kanisani.

**********************************************
*** Shukrani za pekee zikuendee wewe uliyekuwa ukifuatilia simulizi hii kuanzia sehemu ya kwanza mpaka hapa ilipofikia hakika umejifunza mambo mengi sana.
::: Nyuma ya Pazia :::

Simulizi hii imetungwa miaka 4 iliyopita na ilikuwa ni kati ya simulizi zangu za kwanza kuandikia hapa facebook. Haikuwa katika kuhakikiwa na ndio maana makosa madogo dogo yakiuandishi yamejitokeza japo imeeleweka kwa asilimia 98.
**** Mwisho wa simulizi hii ndio mwanzo wa simulizi mpya kaa mkao wa kuisoma nyingine…
~ Mwisho wa Play boy ~

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top