Story: Nililala na maiti 20 ili niolewe na Rais
Sehemu: 6
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633
Ilipoishia…
“Tumuingize ndani. Huyu siyo wa kumbeba ni mateke mpaka ndani kabisa”
Waliendelea kunipiga huku nikijiburuta kwa kutambaa mpaka ndani. Mwili wangu ukawa hautamaniki kwa kipigo. Nilipoingizwa tu ndani nikatazamana na karai kubwa lililokuwa limewekwa viungo vya watu waliofanyia opersheni.Kulikuwa na viungo vya binadamu vya aina nyingi kama, masikio, miguu,mikono,vidole. Vilikuwa tayari kwa kutupwa kwenye moto. Wakanisogeza mpaka karibu na eneo la kuchomea viungo vya mwili. Wakachukua panga nakuanza kutaka kunikata kata kuanzia mikononi.
Songa nayo…
“Nisameheni jamani msinikate! Msinikate!!”
Nilijikuta nikitoa sauti ya kupaza kuomba nisikatwe. Panga kubwa lililokuwa limelowa damu damu lilikuwa mbele ya macho yangu tayari kwa kukatwa katwa Adela mimi. Sikuwa na mtetezi wangu tena. Niliona kifo kikiniita kwa mara ya pili. Kifo cha duniani.
“Baraka mbona unamchelewesha au unamuonea huruma, muadabishe! Hawa hawanaga huruma wanatusumbuaga sana usiku hatulali na watoto wetu vizuri kazi kutuwangia tu!”
Yule kijana niliyesikia akiitwa Baraka akawa amelishikilia panga vilivyo. Aliliinua mpaka juu kwa lengo la kunikata kata. Akalishusha nakunikata mkono wangu mmoja wa kushoto. Mkono ukanidondoka mpaka chini.Maumivu makali yakatawala ubavu wote wa mwili wangu. Maumivu yaliochanganyikana na damu damu. Baraka alikuwa na hasira sana kwani baada ya kunikata mkono mmoja nilishangaa akihamia na mkono mwingine.Akaukata! Alinichakaza mikono yote miwili. Damu nyingi zilitapakaa chini kukawa hakufai. Wale wanaume waliokuwa na Baraka wakakimbia nje nakumuacha Baraka akiendelea kunikata kata vipande vya mikono vilivyokuwa tayari vimesalimiana na sakafu. Sauti ikanikatika Adela mimi.Kwikwi ikanibana.Nikaamini sasa mwisho wa uhai wangu unakwenda kuisha. Mwisho wa kuishi maisha ya kichawi na duniani kwa ujumla. Nguo zote alizokuwa amezivaa Baraka zikawa zimelowa tapatapa kwa damu yangu mimi iliokuwa ikimrukia pindi alipokuwa akinikata kata viungo vyangu. Nguo zikanona damu.Tepetepe!
“Baraka niache, usiendelee kunikata Baraka?”
Nilijitahidi japo kutoa sauti kwa ukali kumsema Baraka lakini haikuwezekana. Sauti yangu ilikuwa bado ya chini sana huku nikihisi koo kujaa na damu damu. Baraka akahamia miguuni mwangu akiwa na panga lake. Akaichabanga miguu yangu yote miwili kuanzia mapajani. Ikakatika vipande vipande. Nikabakiwa kiwiliwili. Kiwiliwili cha kutokuwa na miguu yote wala mikono. Baraka akalitupa panga lake pembeni. Akainama chini kulikokuwa kumetapakaa damu ovyo. Akaanza kukusanya viungo vya mwili wangu kimoja baada ya kingine.Akili yangu nikaihamishia upande wa pili kulipokuwa na lile karai la viungo vingine pembeni yangu. Nikajua dhahiri Baraka atavitupia viungo vyangu mule ndani ya karai. Hakufanya hivyo.Akasonga! akaelekea mpaka kwenye tanuru lililokuwa likiwaka moto nakutupa vipande vya miguu yangu. Akarudi tena mpaka eneo nililokuwa nakukusanya vipande vipande vya mikono yangu nakuvipelkeka tena kwenye tanuru kuvitupa viungue na moto. Niliumia sana moyo. Yale maumivu niliokuwa nayo nilijihisi kuishiwa kabisa nguvu za kichawi. Mwili ulinitetemeka kila nilipokuwa nikiona moto ulivyokuwa ukipamba. Safari hii Baraka akainama nakuchukuwa lile panga lake kwa mara ya pili. Akanifuata nakunishika kichwa changu.
“Wewe si mchawi? Haya Sali sala zako za mwisho za kichawi. Mpumbavu mkubwa wewe kabla sijamalizia kiwiliwili chako!”
Alichukuwa kichwa changu nakutelezeshea panga katika shingo. Nikahisi kama koo likitaka kuachana na mwili. Akaniinamisha kwenye karai kwa nguvu. Uso wangu wote ukasalimiana na viungo vya kwenye karai. Akaniinua nakunirudishia katika karai kwa mara ya pili. Mwili wangu ukashtuka ghafla nakutetemeka mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Nikajihisi maumivu kunipotea ghafla. Ushujaa! Akili yangu ikawa imeshasaidiana na macho kutambua kuwa miili ya watoto wachanga waliokufa kwa bahati mbaya ipo ndani ya lile karai. Imechanganyikana na viungo vya watu wazima tayari kwa kuchomwa moto.
“Adela, hii ndio dawa yetu ya kutukinga tuendapo huko mochwari. Na nyama hii ya mkono wa mtoto mchanga tuliipata huko huko mochwari. Ni tamu sana shika kula!”
Nikayakumbuka maneno yale aliokuwa akiniambia Jamila kabla hatujaja huku mochwari. Maneno juu ya kula ile nyama ya mtoto mchanga. Baraka aliponiinamisha kwa mara nyingine kabla hajaniinua meno yangu yakawa yameshaibuka na kipande cha mkono wa mtoto mchanga kilichoshikana na mwili. Nikatafuna kwa hasira kali. Kadri nilivyokuwa nikitafuna ndivyo na mwili wa Baraka ulivyokuwa ukikosa nguvu. Akalitupa panga lake nakudondoka chini akiyumba yumba kwa kulegea miguu. Akaanza kutapa tapa mithili ya mgonjwa anaeyeugua ugonjwa wa kifafa. Nikazidisha kuitafuna ile nyama kwa hasira.Punde giza likatanda. Mwanga wa kichawi ndio ukashika nafasi yake.Macho ya kichawi yakanitoka upya yakiachana na macho ya kidunia. Nikaweza kuangaza kona ya chumba. Nikashuhudia kumuona Jamila akisimama kwenye kona na upande mwingine nilimshuhudia Sophy na yeye akisimama wakininyooshea vidole kwa kuvikaza. Macho ya ukali na kichawi ndiyo yalikuwa yakiwatoka. Midomoni mwao walikuwa wamejaa damu hali ilioashiria huenda walikuwa katika himaya nyingine ya kutafuna nyama na wametumwa kuja kuniokoa. Kwa mwendo wa maringo huku wakiwa uchi wakanifuata mpaka karibu.
“Iku Adela! Iku sana!”
Kwa kawaida ya wachawi neno ‘Iku’ ni la kutia nguvu sana. Na ukiambiwa ‘Iku’ unaweza kufanya chochote ni kama nguvu za kichawi zinakuongezeka mara mbili yake. Jamila na Sophy wakaniacha na kumfuata Baraka. Wakamnyonya mdomoni mwake sambamba nakung’ata shingo yake kwa kumuachia damu damu kama ishara ya kumpumbaza. Baraka akasimama.Wima! Akawa kama tayari wanajuana naye ghafla. Wakanifuata mpaka karibu na karai lililokuwa mbele ya uso wangu. Jamila akatoa miguu miwili akaishika na Sophy nayeye akatoa mikono miwili akaishika.
“Iku Adela, Iku”
“Iku”
Nikaitikia na mimi. Sophy akatoa kitambaa pembeni ya mkono wake nakutoa dawa.Wakaanza kusaidiana na Baraka kunibeba wakitaka kunipachika miguu. Kwa kawaida mchawi anaweza kukuunga vipande vya mwili kwa kutumia unga unga uitwao ‘CHAYA’ Unga unga huu una rangi kama ya dhahabu na unapatikana katika mizizi ya miti ya mibuyu pekee. Ile miti minene kuliko yote. Jamila na yeye akatoa kitambaa katika mkono wake uliokuwa umefungwa chaya. Akaninyunyizia mikono yote kisha akaninyunyuzia na miguuni wakaiunga.Nikapona!
“Inuka Adela? Inuka?”
Niliweza kuinuka. Sikuweza kuyasikia maumivu yeyote tena. Zile damu damu nilizokuwa nazo zikayeyuka kutokana na nguvu ya dawa ya chaya. Nikawa Adela yule mchawi upya. Adela mwenye nguvu za kichawi mara mbili yake. Tukaongozana wote mimi,Jamila,Sophy na Baraka mpaka kwenye kona nakuyeyuka.
***************
“Oiyeee! Adela tulimwana mnogie Oyieee!! Izee akunu na Baraka Oiyeee!!”
Nilishangaa kukuta idadi ya wachawi ikiwa imeongezeka mara mbili yake. Walikuwa wakinena kwa lugha yao ya kichawi. Walikuwa wakiinua mikono yao juu iliokuwa imeshikilia utumbo wa binadamu. Kwa kawaida ya wachawi, mwenzao anapokuwa amenusurika kukamatwa kwa uchawi huwa wanaitana wachawi kutoka pande zote za jirani kusherekea pamoja na kujazana nguvu nyingi za kichawi. Na huwa wanatoa kafara ya watoto kumi na sita hadi ishirini inategemea na idadi ya wageni. Huyatoboa matumbo ya watoto na kutoa utumbo. Hugawana kila mmoja nakuongea kwa kushukuru huku akiwa amenyoosha mkono mmoja uliojaa utumbo kiganjani mwake. Kwa kipindi hiki mimi ndiye nilikuwa nikifanyiwa sherehe hiyo ya kukaribishwa upya kutokana na kunusurika kufa.
Wachawi wenzangu wakatuzunguka mimi na Baraka huku wakiwaacha Jamila na Sophy. Kundi la wachawi wakiongozwa na baba Jamila wakashusha ule utumbo mikononi mwao mpaka chini kabisa. Wakatandaza ule utumbo.Ukatapakaa!
“Kanyageni hapa Adela! Kanyaga?”
Aliongea baba Jamila. Nyuso yake ilikuwa na furaha sana. Baada ya kukanyaga akanisogeza mpaka pembeni kisha akamuamuru Baraka alale chini.Alalie ule utumbo kama kitanda.Kundi la mabinti wakaja kila mmoja akiwa ameshikilia bakuli kubwa na sindano kubwa kama zile za kushonea magunia. Wakaanza kumtoboa Baraka mwilini mwake. Wakamtoboa kila kona ya mwili wake. Damu nyingi zikamtoka Baraka kupitia sehemu alizotobolewa. Wale mabinti wakakinga zile damu kila zilipokuwa zikitomka Baraka. kila mmoja akajaza damu katika bakuli lake. Baraka alilia sana.Akawa mwembamba sana kwa kukauka damu. Hakuwa na nguvu ya kuinuka wala kufanya chochote kutokana na kuwa tayari katika himaya ya kichawi. akapoteza fahamu kabisa.
“Adela? Shika kisu hiki?”
Baba Jamila akanikabidhi fupa kubwa lenye makali ambalo huliita kisu. Akanishikisha.Hofu ikanitanda!
“Adela? Unatakiwa umtoe utumbo wake wote nje halafu utaanza kuula wewe na kisha utanipa mimi na wageni wetu hapa utamkatia kila mmoja. Sawa?”
****************************************
***** Je Adela atafanikiwa kumtoa utumbo Baraka nakuula? Nini hatma ya Adela katika maisha yake ya kichawi?
**** Simulizi inaendelea kunoga, tegemea utamu zaidi kila itakapokuwa inaendelea. Gonga LIKE na SHARE ili iwafikie wengi zaidi nao wajifunze kitu. Kumbuka LIKE na SHARE nyingi zinafanya Simulizi hii iwafikie watu wengi waguswe kama ulivyoguswa wewe.
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.