Unknown Unknown Author
Title: SIMULIZI: NILILALA NA MAITI 20 ILI NIOLEWE NA RAIS SEHEMU YA KWANZA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Story: Nililala na maiti 20 ili niolewe na Rais Sehemu: 1 Mtunzi: Andrew Carlos Simu: +255 713 133 633 Machozi yangu yaliendelea kunibubuji...

clip_image002Story: Nililala na maiti 20 ili niolewe na Rais
Sehemu: 1
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633

Machozi yangu yaliendelea kunibubujika katika paji la uso wangu mithili ya maji yakifuata mkondo wake. Niliendelea kugalagala chini huku nikiwa sijitambui. Kwikwi ya ajabu ilioambatana na kukohoa pasipo na mpangilio ilikuwa imenibana vilivyo. Sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuwa nikikishuhudia mpaka pale niliposhikwa mkono na jirani zangu niweze kumwaga mchanga wa mwisho katika kaburi kubwa. Kaburi refu lililokuwa limechimbwa na majirani wema kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama yangu mpendwa, mama Adela. Mama aliokuwa ameniacha mimi mtoto pekee tangu alipofariki baba miaka mitatu iliopita na kutuacha katika kipindi kigumu cha kutegemea milo miwili kwa siku.
“Umeniacha mkiwa mama, Niacheniii…?” Watu kibao waliokuwa wakionesha sura za huzuni walikuwa wamenizunguka. Ni mchungaji pekee ambaye alikuwa mbele ya uso wangu akiwa ameshikilia biblia. Nilianza kutapatapa kwa uchungu. Kutapatapa kwa kuendelea kumlilia mama yangu.
Ghafla nilitekwa na nguvu za ajabu katika mwili wangu. Nikajikuta nimeyatoa macho ya ukali kuwaangalia wale wakina mama waliokuwa wamenishika. Mmoja wapo alionekana kuwa na ukali dhidi yangu. Hilo sikulistaajabu, kwa kutumia meno yangu niliweza kuwang’ata wote wawili mikononi mwao na ndio ukawa mwanya wa mimi kuchoropoka na kudumbukia katika kaburi la mama yangu. ‘Tiii’ nikasimama juu ya jeneza. Kamwe sikutaka kuyabinua macho yangu kutazama juu nilipotoka. Nguvu ya ajabu ikanishika na kuendelea kunitawala katika mwili wangu, nilijikuta nikifungua lile jeneza lililoupumzisha mwili wa marehemu mama yangu kipenzi, mama Adela pasipo woga wowote.
“Mama? Mama? Amka mama yangu japo nikuone tena kwa mara ya mwisho mama?”
Niliendelea kulia kwa uchungu huku mikono yangu miwili ilikuwa imeng’ang’ania uso wa mama yangu sambamba na kichwa chake kikikaribiana kabisa na cha kwangu.
“Mama? Hutaki kuamka? Mie nitaishi na nani tena mama yangu?”
Hasira ilinizidia mara mbili ya awali. Ilinibidi niutoe ulimi wangu nakuudumbukiza katika mdomo wa mama yangu. Nilichukua mikono yangu nikaisogeza mpaka masikioni mwa mama kisha nikamtoa pamba masikioni mwake nakudumbukiza vidole vyangu. Nilivuta pumzi yangu kwa kasi nikidhani huenda atashtuka. Hola! Kadri nilivyozidisha kuvuta pumzi ndivyo na harufu kali ilikuwa ikinirudia kutoka mdomoni mwa mama. Nikajihisi mwili wangu unabadilika kwa haraka zaidi. Ile mikono ambayo niliitumia kumuingizia vidole masikioni mwa mama yangu sasa ikawa imebadilika rangi na kuwa na maji maji mithili ya rangi ya kijani kijani.
*******
“Hapa ni wapi? Na mama yangu yuko wapi?”
“Nyamaza na utulie kimya Adela wewe?”
Woga ulianza kunitanda kwa ghafla. Sauti kali ya kike ilikuwa imetingisha ngome ya masikio yangu baada ya kunitaja jina langu.Mwili wote ukaendelea kulowana si kwa maji bali kwa jasho langu mwenyewe. Sikujua sababu ilionifanya kufika katika eneo hili. Eneo lililokuwa limejaa maajabu ya kila aina. Hakukuwa na nyumba hata moja bali watu walikuwa wakipishana wenyewe tena walitembea wakiwa hewani. Si magari wala nyumba la hasha! hazikuwepo. Hakuna hata mmoja aliokuwa amevaa nguo zaidi yangu japokuwa nguo nilizovaa zilikuwa zimenipauka na kuchakaa kwa vumbi na damu damu lililogandia. Nilijihisi mwili wote kuishiwa na nguvu sambamba na kizungu zungu huku macho yangu yakionesha kutoshirikiana katika kumsikiliza mama aliyekuwa mbele ya macho yangu.
“Adela unakumbuka mara ya mwisho ulichokuwa ukikifanya?”
Alirudia jina langu kiufasaha hali iliyonitia woga mara mbili yake huku nikijiuma uma kwa kujibu.
“Hapana sikumbuki”
“Hukumbuki?”
“Ndio sikumbuki na niambieni kwani nilifanya nini na hapa ni wapi mbona sielewi?”
“Unawaona wasichana wenzako kule na kule wanaozunguka wakiwa uchi?”
Haraka haraka niliyazungusha macho yangu kutazamana kinachoongelewa na huyu Mmama.
“Ndio nimewaona”
“Hawa wote hawana wazazi kama ulivyokuwa wewe na hapa unapowaona mchana huu wote tupo nao na ikifika usiku kila mmoja anaenda kazini”
“Kazini? Ndio wapi na ofisi gani hizo za usiku?”
“Eeeh he heee!! Embu wacha kunichekesha Adela. Wewe ulikuwa umeshapoteza uhai ukiwa ndani ya kaburi la mama yako pindi ulipokuwa unamlilia. Na hapa ninavyoongea na wewe si mtu hai bali ni mfu”
“Mfu? Inamaana nilishakufa nikazikwa?”
“Ndio Adela, wewe ni mfu. Mjini kote wanajua kuwa ulishakufa toka kipindi kile ulichodumbukia katika kaburi la mama yako na leo ni siku ya tano umezinduka hapa kwetu. Na ni sisi ndio tuliokupa nguvu za ajabu na kuweza kuishawishi akili yako ifanye vile mpaka kufikia hatua ya kumnyonya mama yako ndimi huku ukimdumbukiza vidole vyake katika masikio yake. Wale wadada unaowaona kule ndio waliofanikisha zoezi zima la kufanya mpaka upo hapa.”
“Miiimi?”
“Ndio wewe Adela na hapa ninavyokwambia wamezika gogo tu tena pembeni ya kaburi la mama yako wakidhani wamekuzika wewe!”
Machozi ya uchungu yalianza kunitoka. Nilijitahidi japo kurudisha kumbukumbu lakini kichwa changu kiliishiwa na uwezo wa kufikiri kabisa. Nilijihisi akili na macho kukosa ushirikiano kabisa. Nilitumia mikono yangu kujipangusa machozi lakini nilistaajabu mikono yangu kuwa na damu damu.
“Adela?”
“Abee!!”
“Umeingia kwenye himaya yetu huku na ni lazima ufuate mila na tamaduni za huku kwetu hayo mengine ya duniani yaache kama yalivyo sawa? Huna mama huna baba wala mume na hata watoto huna hilo tunalitambua na ndio maana siku zote tulitamani kuwa na mtu kama wewe na leo hii upo mikononi mwetu.”
“Hapana mie nataka kurudi nilipotoka nirudisheni tafadhali, nirudisheniii?”
Hasira zilifika kikomo lakini hazikusaidia chochote ndani ya himaya hii ya kufikirika. Nilijiangalia mara mbili mbili umbo langu kwa jinsi lilivyokuwa la kuvutia. Weupe wangu uliokuwa ukiwakosesha usingizi wanaume wengi waliokuwa wakiishi maeneo ya karibu na nyumbani sasa nilikuwa nikiushuhudia ukiharibika. nilijutia hata kwanini nilikataa kuolewa wakati nilipokuwa nikiishi na mama. Maneno ya mara ya mwisho ya mama yangu kuwa nitulie tu nitapata mume mwema sasa nikawa nikiyajutia nakuona dunia chungu. Posa ambazo nilizikataa kwa wanaume zaidi ya watatu waliokuja nyumbani kutaka kunioa ndizo ziliniongezea hasira zaidi.
“Mama nataka unirudishe duniani, nakuomba tafadhali?”
“Unajua Adela wewe ni mwanamke ambaye karibu kila kitu tumefanana na hata mimi nililetwa na hawa wachawi wenzangu pasipo kujijua mpaka huku na uzuri wangu niliokuwa nao. Tena wewe una bahati sana wamekuleta wanawake wenzako ukiwa tayari umeshakufa duniani. Mimi walinileta wazee kabisa na siku ya kwanza nilipofika nilichezewa sana mwili wangu ikiwa ni pamoja na kubakwa mfululizo na wazee. Kila ilipofika usiku ilinibidi ni lazima nilalae na wazee zaidi ya kumi na tano kwa usiku mmoja. Mwanzoni nilipata sana shida lakini kwa sasa nimezoea mwenzako na mpaka nimekuwa kiongozi wa wasichana wote wanaoletwa huku na mimi ndio wazee wamenipa uongozi wa kuhakikisha nawapa kazi za kufanya wasichana wapya kila inapofika usiku sambamba na kuwajaza nguvu zetu za kichawi. Kwanza niambie upo tayari kufanya nitakayokupa kisha nikufanyie mpango urudi duniani?”
“Ndio mama nipo tayari hata sasa hivi”
“Unatakiwa ulale na maiti ishirini huku kila moja ukiivua na kuichezea viungo vyake vya siri ikiwa ni pamoja na kuzinyonya, kuzilamba masikioni na midomoni kama wafanyavyo wapenzi wanaopendana huko duniani, sawa?”
“Hapana, hilo siwezi, siwezi nibadilishie adhabu”
“Mwanangu Adela hiyo siyo adhabu hiyo ni njia ya wewe kurudi katika mazingira ya kawaida ili usiwe mfu tena. Adela umenielewa mwanangu?”

***** Je Adela atafanikiwa kukubali kulala na maiti zote na kuzifanya kama alivyoambiwa? Nini hatma yake ya maisha?
**** Simulizi ndio kwanza imeanza, tegemea utamu zaidi kila itakapokuwa inaendelea. Gonga LIKE na SHARE ili iwafikie wengi zaidi nao wajifunze kitu.
**** Simulizi hii ni ya kweli na kusisimua ambayo imemtokea Adela. Itakuwa Inatoka kila siku

*** Simulizi hii inapatikana kwa mauzo ya online. Unaweza kuinunua yote kwa gharama ya shilingi 2500/= tu, ukawa unajisomea nyumbani kila siku mwanzo mpaka mwisho. Kama utahitaji kutumiwa ni inbox kwa kuandika “Maiti 20”
**** ANGALIZO ****
Hairuhisiwi kusoma kwa mtu ambaye anajijua ni muoga. Ukijihisi kila unaposoma mapigo ya moyo yanakwenda kasi, tafadhali acha. Pia si vizuri ukawa unasoma katika mazingira ambayo upo peke yako ama unaishi peke yako katika nyumba hasa nyakati za usiku. Na siyo vizuri kusoma ukiwa maeneo ya beach ama karibu na milima ni hatari sana.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top