POMBE HARAMU YA GONGO YAKAMATWA NDANI YA BUS LA BUTI LA ZUNGU

clip_image002[8]Haya ndio Madumu yenye pombe aina ya Gongo yaliyokuwa yamepakiwa katika Bus la abiria la But la zungu linalofanya safari zake Lindi – Masasiclip_image002[6]Askari wakisimamia zoezi la Upekuzi ndani ya Min Bus Hiyo

clip_image002[14]Kondakta (mwenye sare katikati) alishikiriwa na polisi baaada ya kukataa kumtaja mwenye mzigo huo ambao ulikutwa ndani ya gari lake

Na Elvan J. Limwagu, Lindi

Gari aina ya TOYOTA Min Bus liitwalo BUTI LA ZUNGU lenye Namba za Usajili T510CFM Tarehe 18/8/2013 lilikamatwa maeneo ya Njenga Ndanda na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Ndanda baada ya kupekuliwa na kukutwa na Madumu 5 ya Pombe haramu ya Gongo yakiwa yamefichwa chini ya siti. Madumu hayo amabayo yalifungwa vizuri ndani ya mabox na juu yake kufunikwa kwa mifuko myeusi ya nylon pasipo kutoa harufu kabisa.clip_image002Bus hilo linalofanywa safari zake kati ya Lindi – Masasi lilikamatwa majira yaa 9 alasiri likisafiri kutoka Masasi kwenda Lindi. Baada ya upekuzi mmiliki wa mzigo huo hakujitokeza na Makondakta walishindwa kumtaja mwenye mzigo huo na hivyo Kondakta mmoja aitwaye ALLY alishikiliwa katika kituo hicho kwa kuisaidia Polisi. Bus hilo ambalo lilibeba abiria nikiwemo “mimi” liliruhusiwa kuendelea na safari saa 9:55 alasiri.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post