Unknown Unknown Author
Title: MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA RUANGWA AJIUZURU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz-Ruangwa, Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia(CHADEMA)wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Abdalah Mohamed Mang’onyola...

clip_image003

Na Abdulaziz-Ruangwa,
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia(CHADEMA)wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Abdalah Mohamed Mang’onyola amejiuzuru nafasi hiyo kwa kile alichoeleza kuwa ametingwa na shughuli zake binafsi.

Uamuzi wa mwenyekiti huyo aliutoa jana(jumatano) baada ya kuwatumia wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho ujumbe mfupi kwa njia ya simu akidai kuwa kutokana an kutingwa na shughuli zake hasa za biashara anakosa muda wa kutekelza majukumu ya chama.

Akizungumza kwa njia na simu na mwandishi wa habari hizi kuthibitisha uamuzi huo, Mang’onyola alisema kuwa ameamua kujiondoa kwenye uongozi wa Chadema ili kupisha wanachama wangine wakiongoze chama hicho kwani muda mwingi anatumia kushughulikia masuala yake ya binafsi.

“kwa sababu ya majukumu yangu ya kifamilia na kwamba muda mwingi natumia kufanya kazi zangu sio za chama natamka kuwa najiuzuru uenyekiti kuanzia leo tarehe 14/08/2013 na taarifa hii wapewe wajumbe wa kamati ya utendaji..mwisho wa nukuu ya ujumbe wa simu toka kwa
mang'onyola

Abdalah Mboga mkazi wa mtaa wa Dodoma ambaye ni mwanachama wa Chadema akizungumzia kujiondoa kwa mwenyekiti huyo, alisema kuwa uamuzi huo utakiyumbisha chama kwani kimetokea ghafla na kuwa kwa wakati huo itawachukua wakati mgumu kuziba nafasi hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top