Makamu wa Rais wa serikali ya mpito ya Misri, Mohammed El Baradei ametangaza kujiuzulu hapo jana akihofia athari za hatua ya jeshi la nchi hiyo kutangaza hali ya hatari. Aidha inatarajiwa viongozi zaidi wa ngazi ya juu wa seriali hiyo wanaweza kujiuzulu. Jumuia ya kimataifa imelaani mauaji yanayoendelea nchini humo ambapo katika operesheni iliyozua mapambano baina ya pande zinazokinzana, mwandishi mmoja wa shirika la habari la Uingereza la Sky News, Mick Deane, ameuwawa kwa kupigwa risasi."
Source: Habari kwa ufupi na Magic FM
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.