JWTZ KUSHIRIKI MICHEZO YA MAJESHI AFRIKA MASHARIKI

clip_image001

Wanamichezo 102 toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watashiriki katika michezo ya majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itafanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 05 Aug 13 hadi tarehe 17 Aug 13.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania atakabidhi Bendera ya Taifa kwa wanamichezo hao tarehe 02 Aug 13 saa 8 mchana tukio litakalofanyika bwalo la askari katika kambi ya TwalipoAdministration Unit (TAU) iliyopo mkabala na Chuo cha Uhasibu,       Dar es salaam.

Vyombo vya Habari vinakaribishwa kuchukua matukio katika hafla hiyo ya makabidhiano.

Kwa mawasiliano zaidi tel no_0715 270 236, 0754 270 236

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

SLP 9203

Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post