Unknown Unknown Author
Title: JERRY SILAA, HASHEEM THABEET WAWAHUDUMIA WATU WASIOSIKIA JIJINI DAR, TAZAMA PICHA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akimpa mazoezi ya kusikia mmoja wa wagonjwa....

clip_image001Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akimpa mazoezi ya kusikia mmoja wa wagonjwa.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuwekea kifaa cha kusaidia usikivu mwanafunzi aliyetambulika kwa jina moja la Adrian jana jijini Dar es Salaam.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo alipokuwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Montage Bi Teddy Mapunda (kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya vifaa vya kusaidia usikivu jana jijini Dar es Salaam. Huduma hii ya kijamii ya kusaidia watu wenye matatizo ya kusikia imekuwa ikitolewa kwa ushirikiano wa taasisi za Starkey ya Marekani, Montage ya Tanzania na Serena Hotel ambapo hii ni mara ya tatu tokea wameanza kutoa huduma hiyo.Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akiwa na Mwanzilishi wa Starkey ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin alipotembelea kliniki ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya usikivu hapa nchini iliyoratibiwa na Taasisi ya kusaidia usikivu (Starkey) kwa kushirikiana na kampuni ya Montage ya Tanzania na Serena Hotel jana jijini Dar es Salaam.Mwanzilishi wa Starkey taasisi ya kusaidia usikivu ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin (wa pili kulia) akifuatilia maendeleo ya mgonjwa wa usikivu wakati akipewa mazoezi kufuatia kupatiwa kifaa cha kumsaidia kusikia jana jijini Dar es Salaam.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na waratibu wa kliniki ya kuhudumia watu wenye matatizo ya kutosikia alipotembelea kliniki hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Starkey Judith Robert, Mkurugenzi wa Montage Teddy Mapunda na Mkurugenzi wa Masoko wa Serena Hotel Serafin Lusala.

Picha zote na Frank Shija - MAELEZO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top