Na Abdulaziz Ahmeid,Dodoma
Umoja wa vilabu vya waandishi wa Habari Tanzania umepinga kitendo cha chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) jimbo la Mufindi kusini kuandika barua ya maombi ya fedha na kutaka ushirikiano na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) katika ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya kifo cha Daudi Mwangosi .Akitoa tamko kwa niaba ya bodi ya UTPC jana, Makamu wa Rais UTPC, Jane Mihanji wakati Akifunga mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho ya Katiba ya UTPC uliyofanyika Mjini Dodoma
Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutumia vifo kama mtaji wa kisiasa.
“..Sisi kama UTPC tunatoa tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie kifo cha Daudi Mwangosi katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na suala hilo au zoezi hilo la kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa kufanywa na chama hicho’ Alisema Mihanji.
Alisema ujenzi wa mnara huo ambao unaotarijiwa kufanywa na Chadema si halali na hivyo kuacha kutumia kifo hicho kutafuta umaarufu wa kwenye majukwaa na kuwataka waache wakawaachia wahusika wenyewe jumuia za waandishi wa habari ambao ndiyo wenye mamlaka na si vinginevyo.Mihanji alisema kuwa, Mwangosi hakuwa mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu katika tasnia ya habari
“Kwani yeye kufuatia mauaji yake hakuwa katika harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo wenye mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni wahusika ambao ni wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.
“UTPC ndiyo wenye mamlaka ya kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho kwahiyo ni vema swala hilo waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo wahusika kwahiyo tunajua nini tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwa hiyo tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho swala hilo liachwe na tuachiwe wenyewe” Alisema makamu wa rais huyo.
Mwangosi alikuwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Chanel ten
Mkoani Iringa ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo (Iringa Press Club) ambapo ameuawa akiwa mikononi mwa jeshi la polisi sep 2 mwaka jana.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.