Naibu Waziri wa Tamisemi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa Madawati toka Benki ya NMBWananchi wa kijiji cha Nachiungo wakiwa katika hafla fupi ya kupokea madawati yaliyotolewa na NMBMbunge wa jimbo la Ruangwa nae akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo kwa ajili ya shule ya Ntawilile iliyopo katika kata ya ChienjeleMadarasa mawili ya shule mpya ya Nachiungo yaliyojengwa na kijiji Hicho kupunguza umbali mrefu uliopo kwa watoto kufuata shule katika kata ya Narungombe wilayani Ruangwa na NMB kusaidia madawatiWanafunzi wa shule ya Ntawile wakisubiri kupokea madawati
Na Abdulaziz Video,Ruangwa
Wananchi wa wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, wametakiwa kuwapeleka watoto wao shuleni pamoja na kuwahimiza kuhudhuria madarasani, ili kupata elimu iliyokusudiwa kwa lengo la kuwaandalia maisha bora ya baadaye.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa elimu TAMISEMI Kassim Majaliwa, wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mtawilile, Nachiungo na Lipande kwa nyakati tofauti wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 74 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotoleawa na Benki ya NMB kwa shule za msingi za vijiji hivyo.
Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa elimu
inajitahidi kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu kwa kutoa
misaada ya madawati, nyumba za walimu na madarasa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wanakuwa ktk mazingira yasiyo wakatisha tamaa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Agnes Hokororo akipokea madawati hayo, amempongeza Naibu waziri huyo kwa juhudi zake za kutafuta misaada kutoka kwa wadau mbali mbali wa elimu na kwamba kupatikana kwa madawati hayo 74 kumesaidia kupunguza upungufu mkubwa wa madawati 3,000 inaoikabili wilaya hiyo ya Ruangwa.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.