YANGA WASHINDI KWA NIDHAMU, YONDANI MCHEZAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA 2013

clip_image002Kipre (katikati) wakati akipokea tuzo yake usiku huu. Kushoto ni Waziri Dk Fenella na kulia Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom, Kevin Twisa.

BEKI wa Yanga SC, Kevin Patrick Yondan ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/2013 na kuzawadiwa donge nono la Sh. Milioni 5.
Hata hivyo, katika hafla ya kutoa zawadi za washindi wa Ligi Kuu msimu uliopita kutoa wadhamini, Vodacom Tanzania zilizofanyika katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam, usiku huu, Yondan hakuwepo na tuzo yake alipokelewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.

Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange akimpokelea tuzo King Kibaden, aliyekuwa bosi wake msimu uliopitaMjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Mussa Katabaro akipokea hundi ya Sh. Milioni 70 za ubingwa Ligi Kuu.Mapacha; Kipre Tchetche (kushoto) akiwa ameshika tuzo yake kwa pamoja na pacha wake, Kipre BalouNidhamu; Katabaro akiwa na Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako wakati wa kupokea tuzo ya Nidhamu.Kipa bora; Kocha wa Kagera Sugar, Jumanne Challe akimpokelea tuzo kipa bora Ligi Kuu, David BurhanMchezaji Bora; Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto akimpokelea tuzo mchezaji bora wa Ligi Kuu, Kevin YondanWashindi wa tatu; Mwakilishi wa Simba SC, Said Tulliy akiipokelea klabu hiyo hundi ya Sh. Milioni 25 kwa kushika nafasi ya tatuMwenyekiti wa Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka akimpokelea tuzo Rajab Zahir

Yondan ambaye alikuwa katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, yuko kwenye kambi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipa chipukizi wa Tanzania Prisons FC ya Mbeya, David Burhan alishinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu na kupewa Sh. Milioni 5, wakati mfungaji bora, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast  wa Azam FC alipewa Milioni 5 pia na Fully Maganga wa JKT Mgambo alipewa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu na kuzawadiwa Milioni 5. 
Kocha mpya wa Simba, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameshinda tuzo ya kocha bora kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Kagera Sugar msimu uliopita na kuzawadiwa Milioni 7.5 sawa na refa bora, Simon Mbelwa.
Yanga SC pamoja na kuzawadiwa Sh. Milioni 70 za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, waliongezewa Milioni 15 kwa kuwa timu yenye nidhamu zaidi kwenye ligi hiyo msimu uliopita, hivyo kuondoka na jumla ya kiasi cha Sh. Milioni 85.
Azam FC washindi wa pili kwa msimu wa pili mfululizo, walizawadiwa Sh. Milioni 35, Simba SC washindi wa tatu Milioni 25 na Kagera Sugar washindi wa nne walipewa Milioni 20.

Picha ya pamoja; Washindi wa tuzo mbalimbali za Ligi Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmiMeneja wa Azam FC, Jemedari Said akipokea Hundi ya ushindi wa pili, Sh. milioni 35Mzigo kachukua Jemedari; Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi kulia akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Coastal, Steven MguttoBanana Zorro na B Band walitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzoWaandishi wa Habari

Kwa upande wa zawadi za wachezaji wa timu za vijana za klabu za Ligi Kuu, Hamisi Saleh (JKT Ojoro), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Chande Magoja (Mgambo JKT), Tonny Kavishe (Mgambo JKT) na Rajab Zahir (Mtibwa Sugar), wote wamezawadiwa Sh. Milioni 1 kila mmoja.

Zawadi za wachezaji wa timu za vijana, walizozawadiwa kwa kuzichezea mechi nyingi timu zao za wakubwa katika Ligi Kuu, zimetoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.

PICHA KWA HISANI YA BINZUBERY

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post