VIJIJI TISA HALMASHAURI YA WILAYA LINDI VYANUFAIKA NA MRADI WA MKUHUMI

mkuhumiMratibu wa Shughuli za Hewa Ukaa kutoka MJUMITA akimkabidhi fedha za Malipo ya majaribio ya MKUHUMI kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Makumba wilayani Lindi

clip_image002Bw. Selemani Kitenge, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nandambi kilichopo Halmashauri ya Manisapaa ya Lindi akionesha fedha za majaribio ya MKUHUMI TZS 49,642,000/= ambazo ziligawiwa kwa wanakijiji wote 731 (na watoto) kila mmoja TZS 40,000/= na kiasi kilichobakia kimetumika kuanza ujenzi wa zahanati ya kijiji (picha hii hapa chini) ambao unaendelea kwa kasiclip_image002[17]

clip_image002[19]Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Makumba (Wilaya ya Lindi vijijini) iliyojengwa kupitia mradi wa MKUHUMI

Na Abdulaziz Video

WANANCHI 11,914 wa vijiji tisa kati ya 425 katika Halmashauri ya

wilaya ya Lindi,wamenufaika kupata Sh,235,053,000/- zikiwa ni mgawo wa malipo yaliyotokana na uuzaji wa majaribio ya Hewa Ukaa, kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Hayo yameelezwa na kiongozi wa mradi wa kuhifadhi misitu (MKUHUMI) mkoani hapa, Nuru Nguya,alipokuwa akizungumza Na Glob hii Ofisini kwake, kijiji cha Kinyope, kata ya Rutamba Wilaya na Mkoa wa Lindi.

Nguya amesema mgawo huo, umetolewa kwa wananchi hao kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2012 na mwaka huu, ambapo kila kijiji kilipata mgawo wa fedha hizo kutokana na idadi ya ukubwa wa maeneo yao.

Ametaja vijiji vilivyonufaika na mgawo huo,ikiwemo idadi ya watu na
fedha walizopata kwenye mabao kuwa ni,muungano iliyo na watu wapatao 2,583 (Sh,51,000,000), huku Nandambi na Kiwawa vyenye wakazi wapatao 1,634 vimepata Sh,98,000,000/-kwa kila kimoja (Sh,49,000,000.).

Vingine ni, Mkombamosi watu 2,256 (Sh,32,000,000.), Ruhoma watu 475 (Sh,21,810,000), Kinyope wakazi 2,322 (Sh,12,600,000.) Mkanga moja 758 (Sh,8,375,000.), Likwaya iliyo na wakazi 66 (Sh,7268,000) huku Milola magharibi 1,468 iliyoambulia kiasi cha Sh,4,000,000/-

“Vigezo vilivyotumika katika mgawo wa fedha hizi za Hewa ukaa, kuliangaliwa ukubwa wa maeneo na miti iliyopangwa kwa kila kijiji husika” Alisema Nguya

Akasema kupatikana kwa mgawo wa fedha hizo,wananchi wa vijiji hivyo wameweza kufanya mambo mengi ya kimaendeleo, ikiwemo ujenzi wa Ofisi za Serikali za vijiji, Zahanati, ununuzi wa madawati mashuleni, ujenzi wa nyumba bora za kuishi, vyombo vya usafiri kama vile pikipiki, Bajaj na Baiskeli.

Matumizi mengine yaliyotajwa ni pamoja na jamii wa vijiji husika
kujipatia sabuni, ununuzi wa vifaa kama vile viatu (Gambuti) kwa ajili
ya wanakamati wanaofanya doria kulinda misitu.

Kiongozi mkuu huyo wa mradi wa MKUHUMI mkoani hapa, amesema fedha za mgawo huo kwa wananchi wa vijiji hivyo, zimetolewa na nchi ya Norway, ambayo ni mfadhili wa mradi huo wa kipindi cha miaka mine.

Mradi wa MKUHUMI uliopo kwa majaribio katika wilaya mbili za Kilosa mkoani Morogoro na Lindi vijijini,mkoani hapa,ulianza rasmi hapa nchini mwaka 2010 na unatarajia kufikia kikomo chake August 04/2013.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post