VIJIJI KUMI VYA HALMSASHAURI YA WILAYA YA LINDI VYAPATA MSAADA WA MIZINGA 128 YA KUFUGIA NYUKI

clip_image002Wanakijiji wa Kijiji cha Ruhoma Wilaya ya Lindi vijijini wakiwa katika mafunzo ya vitendao ya ufugaji nyuki kupitia mradi wa MKUHUMI.clip_image002[15]Wanakijiji wa Kijiji Ruhoma wakivuna asali kwa mara ya kwanza kwa kuwezeshwa na mradi wa MKUHUMI.clip_image002[17]Wanakijiji wa Nandambi wakiwa kwenye mafunzo ya kupima hewa ukaa katika msitu wa kijiji kwa kuwezeshwa na mradi wa MKUHUMI.clip_image002[19]Wanakijiji wa kijiji cha Muungano wakiwa kwenye mafunzo ya kukabiliana na wanyama waharibifu yaliyoendeshwa kupitia mradi wa MKUHUMI

Na Abdulaziz Video

VIJIJI kumi katika Halmashauri ya wilaya ya Lindi, mkoani hapa,

vimepatiwa msaada wa mizinga 128 ya kufuga nyuki pamoja na vifaa vya kujikingia yenye thamani ya Sh,7,680,000/-kwa lengo la kuwawesha wananchi husika kujiongezea vipato na kujikwamua ki-uchumi.

Hayo yameelezwa na kiongozi mkuu wa Mradi wa Mkuhumi kwa mkoa wa Lindi, Nuru Nguya, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo.

Mafunzo hayo yaliyowashirikisha wadau toka mikoa mitatu ya
Lindi, Mtwara na Ruvuma yalikuwa na lengo la kupeana mrejesho wa
utekelezaji kwa wadau na watendaji wa Serikali kwa ngazi za vijiji, kata na wilaya.

Nguya akiwasilisha taarifa yake hiyo, mizinga hiyo imegawiwa kipindi
cha kuanzia 2011,2012,2013 na kwamba kila kimoja kimeweza kupatiwa mizinga 12.8.

Kiongozi huyo wa mradi huo wa Mkuhumi,amevitaja vijiji hivyo,kuwa ni pamoja na Milola magharibi,Kiwawa,Ruhome,Kinyope, Mkanga moja, Likwaya, Makumba, Muungano, Nandambi, Mkumba mosi na Ruhokwe.

Amesema licha ya mizinga pia wananchi wa vijiji hivyo,wamepatiwa na vifaa maalumu vya kisasa zikiwemo sare na kofia kwa ajili ya kuziba mwili kukikinga kushambuliwa na nyuki wanapokuwa wanalina (kuvuna) asali.

Nguya amesema lengo la kuwapatia vifaa hivyo, ikiwemo mizinga hiyo ya nyuki na pamoja na wananchi hao kuwaongezea vipato vyao, vitakavyosaidia kuboresha maisha yao. Aidha, alisema mradi huo wa Mkuhumi pia umekuwa ukitoa elimu kwa wananchi wa vijiji vilivyopo kwenye mradi huo,ikiwemo utunzaji na uhifadhi misitu.

Njia nyingine iliyotolewa kwa wananchi hao ni pamoja na mbinu za
kukabiriana na wanyama waaribifu wa mazao,wakiwemo tembo, ngedere, nyani, nguruwe na kima.

Aidha amezitaja mbinu hizo hizo za asili ni pamoja na kuwapatia nyavu
na kuchoma moto vinyesi vya wanyama wakubwa akiwemo tembo.
Mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki zaidi ya 60 kutoka wilaya za
Kilwa,Liwale,Nachingwea,Manispaa,mkoani Lindi,Masasi,(Mtwara) na
Tunduru (Ruvuma) yalifunguliwa na mkuu wa mkoa huo,Ludovick Mwananzila na kufungwa na mshauri wa masuala ya mali asili mkoa Mwinjuma Mkungu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post