Taarifa kutoka barabara ya kilwa zinasema askari wa usalama barabarani walilazimika kusimamisha dala dala la posta-gongo la mboto na kuwaomba washuke haraka na kuwapisha wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda iliyokua njiani kuelekea uwanja wa taifa jijini DSM tayari kuvaa wenyeji wao TAIFA STARS katika mechi ya kwanza raundi ya mwisho kuelekea fainali za CHAN mwakani nchini Afrika kusini.
akizungumza na blog hii askari wa usalama barabarani ambaye hakutaka jina lake kuanikwa hadharani alisema hitilafu ya gari hilo ilitokea maeneo ya kipita shoto(keep left) cha bendera tatu makutano ya barabara za bandarini na kilwa muda mfupi uliopita.
askari huyo amewashukuru abiria waliokuwemo ndani ya daladala hilo ambapo walipoombwa kushuka hawakuleta ubishi kitu ambacho kimewarahisishia askari hao kuendelea na msafara wa waganda hao japo wengi wameona kama fitina za watanzania kutaka kuwavuruga kisaikolojia waganda hao ili wachanganyikiwe na kupoteza mechi yao ya leo dhidi ya STARS wa Tanzania
Mchezo kwa sasa Ni mapumziko hakuna alietingisha nyavu za lango la mwenziwe
KILA LA KHERI STARS
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.