TAZAMA PICHA ZA MATUKIO YOTE YA MSIBA WA MSANII WA VITUKO SHOW

clip_image002POSA

clip_image002[7] 
Mwanadada msanii ''SHERI MWANA'' Akionekana kuwa mwenye uzuni sana baada kuwa kipao mbele kwa kuhangaika na marehemu Hospitalini enzi ya uhai wake, Na huyo mtoto alipakatwa ndiye mtoto wa Marehemu Posa.
Marehemu ''IBRAHIM MOHAMEDI PAZZI'' ''POSA'' ni mzaliwa wa Dar Es Salaam Elimu yake ni ya msingi amesoma shule ya msingi Makutano Mabibo Jijini Dar. Amezaliwa mwaka 1974 na kuiaga dunia mwaka 2013 katika Hospitali ya mwananyamala baada ya kuumwa kwa mda mfupi, aliusumbuliwa na moyo kutanuka pamoja na mapafu kujaa maji, Marehemu POSA ni msanii aliechipukia katika tasnia ya uchekeshaji na kufanya kazi katika kampuni ya Al-Riyamy production kwa mda wa takribani kama mwezi saba, Na kujiengua kwenye kampuni,.. Akaamua kujishughulisha na shughuli hio hio ya uchekeshaji kwa kushirikishwa na wasanii mbali mbali wa comedy hapa nchini.. Kwa wale wasiomfahamu marehemu posa baadhi ya kazi alizo shiriki za kampuni ya Al-Riyamy Productio ni WAKE UP, MACHIMBO na zinginezo, Pia alikuwa kupata airtime katika kipindi cha VITUKO SHOW kinachorushwa na runinga ya CHANNEL TEN. Marehemu ameacha mchumba (Saumu) na mtoto (Rehema) Mwenye umri wa miezi 3.. Amezikwa kijijini kwao MZENGA Dar Es Salaam siku chache zilizopita. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema meponi.

Masai Nyotambofu Mchekeshaji katika kundi la VITUKO SHOW ambae pia ni Director wa blog hii Akiwa katika harakati za kwenda kuuhifadhi mwili wa msanii mwenzie.



Sara Inye!

Wajomba wa marehemu wakiwa katika hali ya uzuni nyumbani kwao na marehemu manzese tiptop Jijini Dar Es Salaam.

Hapa ni baada ya kutia tim kijijini Mzenga mambo yalikua hivi.

Masai Nyotambofu akijadiliana na baadhi ya wasanii kuhusu kusafirisha mwili wa marehemu.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA









Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post