Unknown Unknown Author
Title: TAASISI ZA UMMA ZITUMIE FURSA KULETA KASI YAMAENDELEO - KOMBANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) akifungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi wa ...
clip_image001Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) akifungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi wa Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Na James Katubuka
Uwajibikaji katika Taasisi za Umma nchini ndiyo njia pekee itakayowezeshautekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP) 2011/12-2015/16, sanjari na Malengo ya Milenia (MDGs) .
Kwa kuzingatia hiloSerikali inaendelea kuhakikisha mazingira ya kazi yanaboreshwa iliwatumishi wawe na kasi zaidi kama sehemu ya utekelezaji wa mipango yamaendeleo kwa kutoa huduma bora kwa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (MB) amesema hayo hivi karibuni wakati akifunguamkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano jijini Dar es Salaam.
“Kutokana na kuthaminiwa kwa mchango wa watumishi wa umma katikakuleta maendeleo Serikali nyingi ikiwepo ya Jamhuri ya Muungano waTanzania zimewekeza katika kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma iliwaweze kuwajibika ipasavyo” Mh. Kombani alisema.
Aliongeza kuwa ubora wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa umma ni sualamuhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yoyote, hivyo Tanzania kwakuwekeza katika rasilimali hiyo itapiga kasi zaidi ya kimaendeleo.
Mimi ni miongoni mwa wanaoamini kwamba utendaji mzuri au mbaya waSerikali unahusishwa moja kwa moja na kiwango cha huduma zitolewazona Serikali kwa umma kupitia taasisi zake” Mh. Kombani alitoa angalizo.
Aidha,alisema ukiilinganisha Tanzania na nchi za Barani Asia na Amerikaya Kusini ambazo tuna historia zinazoshabihiana, inaonekana kuwazimepiga hatua ingawa mbinu zilizotumika toka nchi hizo zinakaribiana,hivyo kutokana na uhalisia huo Serikali imefanya jitihada za kuboresha nakufikiri upya namna ya kufikia malengo ya maendeleo haraka husanimchango wa Utumishi wa Umma.
Mh. Kombani alisema kwamba uwajibikaji wa watumishi wa Umma nchinini chachu ya kufikia malengo ya Kitaifa ya Milenia mwaka 2025, ikizingatiwa kuwa malengo hayo yamejikita katika kuleta hali bora zaidi kwamaisha ya wananchi, utawala bora, amani ,umoja na mshikamano nakujenga uchumi imara.
Katika kuchangia hilo, Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Tume ya Mipango nchiniBw. Florence Mwanri alisema mpango huo uliozinduliwa na Serikali mwaka 2011 kwa lengo la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Milenia mwaka 2025, umetoa vipaumbele ambavyo ni kuimarisha Miundombinu, Kilimo, Uvuvi na Misitu, Kuboresha Elimu, na kuendeleza Sekta ya Utalii, Biashara na Uchumi.
Hata hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Dkt. Martern Lumbangaakitoa mchango wake alisema ili kutekeleza mpango huo ipasavyo ni vizuri kujifunza kutoka kwa nchi nyingine ambazo miaka thelathini iliyopita zilikuwa sawa na Tanzania kimaendeleo.
Dtk. Lumbaga aliainisha nchi hizo ni kama vile Jamhuri ya watu wa China, Korea ya Kusini, Vietnam, Cambodia, Botswana na Ghana.
“Utawala wa Kisiasa wa nchi hizi uliweza kuziunganisha Sekta za Ummana Sekta binafsi kutumia Rasilimali muhimu katika kubuni mbinu mbalimbali za kuwavutia wawekezaji wa nje kuwekeza katika sekta nyeti zauchumi zilizoimarisha pato kwa kiwango cha juu” Dkt. Lumbaga alisema.
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Dkt. Lumbanga alisisitiza kwamba Sekta za Umma zinatakiwa kuwa chombo cha kubuni na kuwezesha maendeleo kwa mifumo ya kiufundi, kwa kuzingatia maadili ya kiutawala ili kujenga imani kwa umma na kuhakikisha mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP) unaratibiwa kikamilifu.
Mkuu huyo wa Utumishi mstaafu alisisitiza kuwa sekta ya umma nchini inatakiwa kuwajengea uwezo Watumishi wake ili wawajibike ipasavyo, kuwa na mawasiliano ya kiutendaji yaliyo hai muda wote na kutambua kwamba Utumishi wa Umma upo kwa ajili ya kuwa hudumia wananchi.
Naye Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Bw. Phillemon Luhanjo akizungumzia kuhusu changamoto zinazoukabili Utumishi wa Umma na mtazamo wa Sekta binafsi dhidi ya Utumishi wa Umma nchini, alisema moja yachangamoto ni dhana ya kukubali kubadili fikra na kuleta fikra endelevu zitakazo kuwa chachu ya maendeleo nchini katika nyanja za Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni.
“Sekta binafsi zinatakiwa kushirikishwa katika kuandaa mipango yetu yamaendeleo” Bw. Luhanjo alisema.
Alifafanua kuwa kwa upande wa sekta binafsi zinatakiwa kupewa fursa yakuchangia mawazo endelevu ili mpango wa maendeleo uwe wenye manufaa.
Bw. Luhanjo aliainisha kuwa Taasisi za umma zinatakiwa kufikiri juu ya mahitaji ya wananchi hususani suala la umasikini na kusisitiza Utumishi waUmma lengo lake si kujilimbikizia mali, bali lengo kuu ni kutekeleza malengo madhubuti ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema ili kukabiliana na changamoto zilizopo Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendelea kuimarika, mahusiano na Sekta binafsi yanaimarishwa zaidi, bajeti ya nchi iimarishwe ilikupunguza utegemezi wa wafadhili wa nje na Sekta ya Umma kutambua mchango wa Sekta binafsi katika kuleta kasi zaidi ya maendeleo.
Pamoja na hayo, Katibu Mkuu mstaafu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Joseph A. Rugumyamheto akizungumzia kuhusu ushirikishwaji na wajibu wa Utumishi wa Umma katika kuleta maendeleo nchini alisema jukumu la Utumishi wa Umma katika kuleta maendeleo ya kitaifa limekuwepo toka kipindi cha uhuru mpaka sasa.
Bw. Rugumyamheto alisisitiza Utumishi wa Umma ndio chombo pekeechenye jukumu kubwa la kuwezesha uratibu wa programu za maendeleoza kijamii na kiuchumi hapa nchini.
Katibu Mkuu mstaafu alisema wachambuzi wa masuala mbalimbaliwameandika kuwa Utumishi wa Umma katika kipindi cha Uhuru ulikuwaunazingatia taaluma na ulikuwa ni chombo kilichowajibika kikamilifukutimiza matakwa ya Kisiasa na Kijamii. Hivyo, kwa sasa kasi iongezekezaidi.
Bw. Rugumyamheto aliainisha kuwa kwa sasa Utumishi wa Umma unawigo mkubwa wa uwepo wa wataalamu wengi wenye ujuzi katika fanimbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali, pia matumizi ya teknolojia hususani maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamerahisisha uandaaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusimamia utekelezaji wake, hivyo Utumishi wa Umma uliopo una nafasi kubwa ya kuwahudumia wananchi ipasavyo na kufikia malengo kwa haraka.
Akizungumzia kuhusu hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Vijana nchini Nigeria Dkt. Tunji Olaopa alisema kinachohitajika ni kuwa nampango utakaoiwezesha kuondokana na dhana ya utendaji wa mazoea na kutoka katika fikra ya utamaduni wa kitawala wa kirasimu na kujikita katika mfumo wa ujasiriamali ikiwamo ubunifu katika kushughulikia masuala ya mishahara na masilahi ya watumishi ili kuwajengea morali na uwajibikaji kwa umma.
“Utawala makini na uliojitolea kuutumikia umma ndio nguzo ya maendeleo, na ikumbukwe kwamba Utumishi wa Umma ukishindwa kuwajibika ipasavyo na masuala yote yahusuyo maendeleo yanakwama” Dkt. Olaopaalisema.
Aidha, Dkt. Olaopa aliipongeza Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchizenye sifa ya kuwa na utawala bora unaoheshimika Barani Afrika. Mtafiri Adamolekun katika tafiti yake ya mwaka 2005 aliyoitoa mwaka 2009 kuhusu masuala ya Utawala Barani Afrika imeainisha kuwa Tanzania nimoja kati ya nchi zilizofanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Umma.
Utafiti huo ulihusisha nchi nyingine kama Benin, Burkina Faso, Ethiopia,Ghana, Kenya, mali na Senegal. Akichangia mada,
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Prof. Rwekaza Mkandala alisema Rasilimaliwatu ni msingi wamaendeleo, hivyo ni lazima nchi kuwa na Watumishi wa Umma waliopewa mafunzo bora na ujuzi unaokidhi mahitaji.
Prof.Rwekaza alisema kuwa Watumishi wa Umma wanatakiwa kuwa na uzalendo na nchi yao na wasiohitaji kusimamiwa ili kutekeleza majukumu yao. Alisema “ili Utumishi wa Umma ufanikiwe unahitaji kwenda sambamba na Teknolojia kulingana na mazingira halisi yaliyopo na muda husika, pia unahitaji kuwa na vitendea kazi mahimu kufanikisha hilo ikiwamo mifumo ya kompyuta itakayoiwezesha mifumo mbalimbali iliyobuniwa na Serikali kufanya kazi ipasavyo”.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejjimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu alisema Serikali imeainisha maeneo matano ya utekelezaji wampango wa maendeleo ambayo ni kilimo, elimu, nishati, miundombinu na rasilimali na hivi sasa kuna chombo kitakacho simamia na kutathmini mipango itakavyotekelezwa, chombo hicho kinaitwa Presidential Delivery Bureau.
(Mwandishi WA makala hii ni Afisa Habari, Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma)






























About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top