Unknown Unknown Author
Title: RIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA KUMI NA TANO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK MTUNZI: Emmy John Pearson SEHEMU YA KUMI NA TANO Alipochoka kunichekesha nisiyecheka akatoweka na kwenda bafuni....

FACERIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK
MTUNZI: Emmy John Pearson
SEHEMU YA KUMI NA TANO
Alipochoka kunichekesha nisiyecheka akatoweka na kwenda bafuni. Nikabaki chumbani peke yangu! Hapo likanivamia ghafla wazo la kutoroka! Funguo zilikuwa mlangoni! Kwanini nisikimbie? Nilijiuliza. Hapo sasa ndipo nikagundua kwanini sina ubavu wa kukimbia. Huyu bwana alikuwa anahodhi maisha ya mama yangu! Mwalimu Nchimbi.
Nilipotambua hilo nikafadhaika. Nikakiendea kitanda nikajitupa, nikautupa na mkoba wangu!
Ilikuwa lazima nifanye mapenzi na Davis ili kuokoa maisha yake.
Nilifadhaika bila kujua nini la kufanya. Mlango wa maliwatoni ukafunguliwa. Kichwa kilikuwa kizito hata kunyanyuka kushuhudia ni kimbwanga gani kipya atakizua Dokta huyu!
Akajikoholesha kama anayerekebisha koo. Nikaijua nia yake! Nikanyanyua kidogo! Macho wazi!! Yowe la uoga likanitoka kwa nilichokiona.
Hili lilikuwa kubwa kupita yote!
Kilichokuwa mbele yangu ni kiumbe kile kile kinachoitwa Davis.
Lakini sasa hakuwa na nguo. Maungo yake yote yakawa yananidhihaki, japo alikuwa mweusi tii. Lakini ule mwanga pale ndani uliniwezesha kutambua kuwa alikuwa amelowana damu katika viungo vyake vya uzazi, na hiyo damu ilikuwa mbichi na ni kama ilikuwa inaendelea kumtoka lakini ajabu haikuwa inadondoka katika marumaru!
Hapa sasa nilimsahau kwa muda mwalimu Nchimbi, nikauacha mkoba nikakimbilia mlangoni.
Ajabu! Ule funguo haukuwepo tena mahala pake! Dokta akacheka sana huku akinifuata kwa hatua ndogo ndogo!
Nilitegemea huenda nitapoteza fahamu. Lakini hiyo haikutokea niliendelea kushuhudia kiumbe huyu akinifuata.
Nikawa narudi kinyumenyume hadi nikafika mwisho. Davis akazidi kunisogelea. Sasa alikuwa amenifikia!
Akanishika mkono! Kiganja chake kilikuwa cha baridi sana!! Akanitazama usoni, nami nikamtazama. Akaniachia kisha akasonya kwa dharau. Akakiendea kitanda akajirusha pale!
Bado mashuka hayakuchafuliwa na damu mbichi.
Hakika sikuwa tayari kufanya mapenzi na kiumbe kile cha ajabu!! Niliapa!
Muwasho ulianza kama wa kawaida tu katika chuchu yangu moja, nikajikuna, muwasho ukapita.Mara ile chuchu ya pili nayo ikawasha nikaikuna ikatulia.
Sasa zikawa zinawasha zote kwa pamoja, muwasho usiofanana na ule wa kumwagiwa upupu. Huu ulikuwa wa tofauti. Nikatazama kitandani yule Dokta alikuwa amesinzia. Nikaitoa Sidiria yangu ili nijikune vizuri. Nikabaki bila nguo kwa juu. Nikafanya jitihada za kujikuna!! Ile hali ya kujikuna ikautwaa uoga wangu nikahamia katika hisia za raha! Raha ya kujipapasa! Mazito!
Ni heri ningekuwa na mikono mitatu huenda ningeweza kuipinga hali hii. Maana sasa kati kati ya mapaja muwasho ukazaliwa. Niache wapi? Nikune wapi? Nikajiuliza.
Raha ikawa karaha!
Nikaanza kulia huku nagalagala chini. Nilijikunja na kujikukunjua bila mafanikio! Nilihitaji msaada wa hali ya juu! Msaada wa kukunwa!
Mara kama ameshtuka ndotoni yule kiumbe pale kitandani aligutuka. Akasimama akanitazama kisha akachuchumaa. Akanisogelea karibu zaidi. Sikuwa na nguvu mwilini.
Hakuwa na nguo nami sikuwa na nguo!
Kama vile alijua ninapowashwa! Akaanza kunikuna kwa namna ya kupapasa! Nikahisi raha ya kipekee ambayo sijawahi kuipata duniani. Bila kujitambua nikamkumbatia Dokta Davis.
Akaendelea kunikuna! Sasa nilikuwa hoi.
Fanya unalotaka! Ndivyo ningeweza kusema kama angeniuliza.
Lakini hakuniuliza!
Nikajikuta katika ulimwengu wa mahaba mazito! Kama kukunwa hakika nilipata mkunaji!
Muwasho ukatoweka kabisa. Jasho mwili mzima.
Nikapitiwa na usingizi kutokana na uchovu.
*****
Saa kumi na moja alfajiri hapakuwa na Dokta wala nguo zake pale ndani. Nilikuwa peke yangu.
Maumivu kifuani kama niliegemezewa gogo! Maumivu haya yakanikumbusha ndoto za kuota nazini na gogo!
Nikashtuka! Mbio mbio bafuni nikatapika!
Kumbukumbu ya kufanya mapenzi na Davis usiku uliopita ilinijia kichwani!
Yupo wapi sasa shetani yule? Nilijiuliza.
Ile hali ya maungo ya Davis kuwa na damu ilinisisimua na kujiona kuwa sina thamani tena ulimwenguni.
Kama sina thamani, bora nife! Niliamua!
Nitakufa vipi sasa? Hilo likawa swali la kujiuliza. Nikayakumbuka maneno ya dada Suzi. Kuhusu utoaji mimba na madhara yake!
Nikafikia maamuzi ya kutoa mimba! Kisha nitajua nini cha kufanya!
Wakati natoka pale chumbani na kupita mapokezi nilikumbana na swali, "mwenzako bado yupo? Maana tunataka kufanya usafi". Mwenzangu? Mwenzangu nani? Wanamaamisha Dokta Davis. Sikuwajibu nikajongea na kupotea eneo lile.
Nikaamua kurejea nyumbani kwangu. Tayari nilikuwa na taarifa kuwa mama anaendelea vizuri kiafya!
Tumbo! Tumbo! Tumbo lilianza ghafla kuniuma, upande wa kushoto!! Nililalamika sana, dereva wa teksi akaegesha pembeni akaniuliza kulikoni.
“Nipeleke hopitali!! Nipeleke nitakulipa” nilimsihi huku nikizidi kuugulia.
Kama nilivyoomba akaendesha hadi hospitali iliyokuwa jirani. Alikuwa ni kati ya masalia ya watu wakarimu waliobaki hapa duniani. Aliwahi kuwaita manesi. Japo walichelewa lakini walikuwa kunibeba kutoka ndani ya gari lile.
Moja kwa moja nikakimbizwa wodi ya wanawake!!
Nikapatiwa huduma ya kwanza!!
Baada ya muda damu ikaanza kunitoka!! Nilikuwa nimeingia katika siku zangu ama? Nilijiuliza bila kupata majibu!! Mjamzito naingia katika siku zangu!!
Kadri damu ilivyokuwa inavuja ndivyo maumivu yalizidi kupungua na hatimaye kuisha kabisa.
Majibu ya daktari yalikuwa kwamba. Ni tatizo la kawaida tu kwa mwanamke kuumwa tumbo akiwa anaingia katika siku zake. Lakini mimi nilikuwa mjamzito sasa!! Au mimba imetoka. Sikutaka kuondoka na dukuduku. Nilimvuta daktari tukazungumza kinagaubaga.
Akafikia hatua ya kunipima ujauzito!!
Hakuchukua muda mrefu akarejea. Alikuwa hajachangamka na ni kama alikuwa na jambo anahitaji kunieleza.
“Ina miezi miwili sasa!!.” Aliniambia katika namna ya mshangao.
“Ni maajabu wewe kuingia katika siku zako!!” aliendelea. Mimi nikiwa msikilizaji.
“Kwa hiyo ni nini Dokta.”
“Rudi baada ya siku saba. Kama ikiendelea hivyo. Ama la basi utakuwa mshtuko tu.” Alimaliza.
Nikaondoka zangu huku nikiitazama dunia jinsi inavyonizomea.
****
Maria hakushangazwa na hali yangu ya kuvuja damu!! Aliamini ni kawaida tu kwa msichana. Hakujua kama nina mimba!!
Siri nikabaki nayo. Mimi na daktari!!
Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu….damu zinaendelea kuvuja tena bila kukoma!!!! Kazi ikawa ipo kwangu kila mara kubadili nguo zangu.
Siku ya nne, ya tano….bado tatizo likawa lile lile. Mateso sasa!!! Mimba gani hii!!!
Sikuingoja siku ya saba ifike. Nikarejea hospitali.
Daktari alinipokea vizuri. Nikampa kwa siri kiasi fulani cha pesa ili aweze kunihudumia kwa upendeleo.
“Hadi leo bado damu inakutoka?” alishangaa daktari. Nikamthibitishia kuwa bado zinatoka tena mfululizo.
Akakuna kichwa chake chenye mvi nyingi kasha akahamia kidevuni. Na penyewe akajikuna kwa muda.
“Hebu njoo…” akanipeleka katika chumba kingine. Akanipima tena mimba.
Daktari akashtuka!!!
“Kwa mara ya kwanza katika miaka yangu 20 ya kazi!!!” alihamaki.
“Nini? Nini dokta.” Niliuliza.
“Wiki iliyopita ilikuwa na miezi mingapi vile.”
“Miwili ulisema.”
“Sasa imefikaje miezi sita leo???” aliniuliza. Nikahisi kuzizima. Nikakaa chini!!!
Daktari naye alikuwa ana hofu!!
****
Ni kama daktari alikuwa haamini ambacho amekiona, katika mwili wangu na alichokuwa akifanya pale ni kunitoa tu katika hofu. Mabadiliko ya mimba yangu yalimfanya achanganyikiwe.
Tulirejea katika chumba chake cha ofisi. Mazungumzo yaliyokuwepo ni juu ya kuitoa mimba ile.
Daktari alikataa kata kata akidai kuwa mimba ikifikisha miezi sita na msichana akijaribu kuitoa basi lazima atapatwa na matatizo na kuna uwezekano wa kufa.
Maelekezo ya daktari yaliyoambatanishwa na neno KUFA yalinipa ahueni ya nafsi kwa sababu nilikuwa nataka kufa. Sikuwa na ujasiri wa kujiua na hakika nilikuwa naogopa kufa.
Lakini kufa kwa namna anayoitaja daktari hata hakunipa hofu badala yake nikavutika na kumsihi anisaidie kuitoa ile mimba.
Mazungumzo yalikosa kabisa muafaka. Daktari yule alikuwa mbishi sana hakutaka kushiriki katika utoaji mimba huu. Nilipoona daktari huyu amekuwa na msimamo sana niliamua kutumia njia fulani ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Nikaangusha mezani shilingi laki mbili. Akazikataa, nikaaga nikatoka. Niliporejea niliziongeza zikafika laki nne.
Daktari akazikodolea macho, kisha akatazama kushoto na kulia.
“Umekuja na nani?” akaniuliza.
“Mwenyewe!” nikamjibu. Akatazama tena kushoto na kulia kisha akazikwapua zile pesa akazizamisha katika sehemu zake za siri. Nikakwepesha macho.
Akanifanyia ishara ya mkono. Nikamfuata hadi katika chumba kilichokuwa na harufu kali ya madawa. Akakifunga na funguo tukabaki wawili tu! Kimya.
Daktari alikuwa na hofu. Nililitambua hilo. Sikutaka kuuliza chochote.
“Toa nguo zote.” Aliniamuru. Kauli yake ikanikumbusha kauli ya yule Mnaijeria aliyetaka kunibaka kwa kujifanya ananifanyia tiba ya asili. Huyu sasa alikuwa daktari, nikaamua kucheza pata potea. Kwanza nilikuwa natokwa damu. Sidhani kama angeweza kujaribu kunibaka.
Nikaziondoa zote, wakati huo yeye alikuwa amejikita katika kuchanganya madawa yake ambayo sikuelewa kazi yake ni ipi. Nikabaki kumsubiri.
Njoo hapa!! Aliniamuru huku akinielekezea kitandani.
Geuka hivi!! Nataka kukuchochoma sindano. Nikageuka huku nikiwa katika uoga. Kifo! Nilikuwa naogopa kufa.
Nikahisi kitu cha baridi kikinipapasa. Nikauma meno yangu kungoja uchungu wa sindano. Nilingoja huo uchungu lakini hamna nilichohisi.
“Acha kujikaza wewe sindano itakatikia ndani.” Alinigombeza daktari. Nikashangaa hizo lawama zinatoka wapi wakati mimi hata sijajibana. Alipoona simjibu kitu akanichapa kibao. Nikashtuka.
“Mkubwa hivyo unaogopa sindano alaa!!” alinigombeza. Sikumjibu!!
Nikatega tena aweze kunichoma!! Hali ikawa vile vile.
“Sasa mimi nakuchoma hivyo hivyo.” Alichukua maamuzi yake binafsi.
Nikageuka. Nikayasubiri maumivu!!
Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.
“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.
Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.
“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.
Kisha nikamfuata hadi ofisini!
“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!
Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.
Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.
Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!
“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”
“Wenzangu? Wapi”
“Mnaomtumikia”
“Nani?” nilihoji kwa hofu.
“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.
Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.
“Daktari sijui lolote mbona.”
“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!
“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.
ITAENDELEAAAA….

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top