Unknown Unknown Author
Title: NIMECHOSHWA NA WANAUME MASHAROBARO WA TANZANIA....BORA WA NIGERIA WANAJUA KUPENDA"...REHEMA FABIAN
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mlimbwende  aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nig...

clip_image001Mlimbwende  aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga naye ndoa. 

Akichati na mwandishi wetu, kwa njia ya mtandao, Rehema alikiri kuwa na mwanaume huyo ambaye ni mtu mzima na kweli ni mtoto wa balozi huyo.

“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana kunipenda,” aliandika Rehema.

Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.


“Tumepanga kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni huko muda si mrefu,”  aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge la sherehe.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top