Mabadiliko: Jose Mourinho amezungumzia kubadili mfumo wa uchezaji ili kuwafurahisha mashabiki Chelsea
KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba yuko tayari kumaliza desturi ya kukandiwa juu ya mfumo wake wa uchezaji 'kupaki basi' kwa kutumia soka ya kushambulia, ambayo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich anataka.
Kocha huyo Mreno, ambaye ameanza maandalizi ya msimu mpya wiki hii katika kipindi chake cha pili cha kufanya Chelsea, aliingia mzioni katika awamu yake ya kwanza akiwa na iPad.
Mourinho alitaniana na Frank Lampard na Gary Cahill wakati akikinoa kikosi chake kipya huko Cobham mchana.
Kuwa Frank: Baadhi ya nyota wa Chelsea wanaweza kuwa wamepagwa kumuona kocha wao mpya akiongoza mazoezi na iPadKaribu tena, Jose: Frank Lampard na John Terry wanaweza kuwa wamefurahi kumuona Mourinho amerejea ChelseaChini ya maelekezo: Mreno akizungumza na Demba Ba na Gary Cahill huku ameshika iPadVijana wapya: Marco van Ginkel (kushoto) na Andre Schurrle wameanza kazi Chelsea
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Inter Milan mtindo wake uchezaji wa kujihami zaidi ulizaa maswali mengi siku za nyuma, lakini sasa anataka kuimarisha timu na kuwavutia mashabiki kwa soka ya kushambulia.
"Nataka kuwafanya mashabiki wa Chelsea wafurahi – kwa matokeo, kwa mtindo wetu wa uchezaji, kwa uwezo wetu na haiba nzuri ya timu,"amesema.
"Wanatakiwa kujua kwamba, kuna matokeo ya aina tatu katika mechi – ambapo tunaweza kushinda, sare au kufungwa – lakini wakati wote tunajituma kwa kila kitu,".
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.