Unknown Unknown Author
Title: MAWAKALA WA MABASI WAJIPANGA KUSUSIA KITUO, NACHINGWEA–LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Huku kukiwa zaidi ya sh milioni 700 zikiwa zimeanza kutumika katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi ...

stand nach (2)Huku kukiwa zaidi ya sh milioni 700 zikiwa zimeanza kutumika katika
ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha wilaya ya Nachingwea, mkoani
Lindi ambapo zoezi la ujenzi wa kituo kipya cha mabasi wilayani humo
kuanza kujengwa na kutumika katika maeneo ya uwanja wa ndege
stand nach (3)Baadhi ya Abiria leo wametishia kugoma kutokana na Kuzuia tena uwepo wa kituo cha karibu na maeneo ya Mjini kutokana na Umbali uliopo na kituo hicho kipya.

Hali hiyo imetokea leo asb baada ya baadhi ya Abiria kugoma kituo
kipya baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kushirikiana na Jeshi la
Polisi kufuta kituo cha Tunduru ya Leo na kuagiza wasafirishaji wote
kutumia kituo cha Stesheni kuwa cha mwisho njiani kabla kufika kituo
kikuu ambapo kuna umbali mrefu hali inayofanya Abiria wengi kunufaisha watoa huduma za bajaj na Bodaboda huku wengine wakitembea Umbali Mrefu huku wakipita msituni.
stand nach (1)Akiongea na Mtandao huu Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema wilayani humo, Ahmaid Mmow alieleza kuwa hali hiyo imeleta kero kubwa kwa Abiria wanaosafiri kati ya Nachingwea, Masasi, Newala, Lindi na Dar es salaam huku wengine wakisafiri wakiwa na shida mbalimbali za kijamiistand nach (4)Abiria wengi baada ya kuanza kwa stand mpya waliumia sana na umbali na msitu uliopo lakini Halmashauri ilipoanzisha kituo cha Tunduru ya Leo kidogo kilileta ahueni sasa sijui ni kwa nini wamekifuta hali inayofanya abiria wengi kulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 5 hadi stand Mpya na stesheni Hii inaumiza sana hasa wenye wagonjwa

Kufuatia hali hiyo Baadhi ya Mawakala wa Mabasi ya Abiria na Abiria
wamedhamiria kuitisha maandamano ya kuamasisha kutotumia kituo kipya kinachoendelea kujengwa hadi kitakapokamilika kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma muhimu za kijamii ikiwemo mabanda ya kupumzikia Abiria ambalo lipo hatua za ukamilishwaji

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top