Unknown Unknown Author
Title: MAN UNITED WAICHAPA A-LEAGUE ALL STARS IX 5-1!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LEO huko Sydney, Australia, Mabingwa wa England Manchester United wameilaza A-League All Stars Bao 5-1 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa ...

clip_image002LEO huko Sydney, Australia, Mabingwa wa England Manchester United wameilaza A-League All Stars Bao 5-1 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa ANZ uliojaza Watu zaidi ya 83,000 na kumpa Meneja mpya David Moyes ushindi wake wa kwanza.

Bao za Man United zilifungwa na Chipukizi Jesse Lingard Bao 2, Danny Welbeck Bao 2 na Robin van Persie, alieingizwa Kipindi cha Pili, Bao 1.

Kwa mara nyingine tena Wilfried Zaha alionyesha cheche zake na kukosa Bao kadhaa.

Hii ni Mechi ya pili katika Ziara ya Man United huko Nchi za Thailand, Australia, Japan na Hong Kong na katika Mechi ya kwanza waliyocheza huko Bangkok, Thailand walifungwa Bao 1-0 na Singha All Stars.

Kesho Man United wanasafiri kwenda Japan ambako watacheza Mechi mbili ya kwanza ikiwa Jijini Yokohama dhidi ya Yokohama F-Marinos hapo Jumanne Julai 23.

Kisha wataenda huko Jijini Osaka watakapocheza na Cerezo Osaka.

Cerezo Osaka ni Timu ya zamani ya Kiungo wa Man United anaetoka Japan, Shinji Kagawa, ambae kwa sasa yuko kwao Japan na atajumuika na wenzake huko Japan.

VIKOSI VILIVYOANZA:

A-LEAGUE ALL STARS IX: Covic, Bojic, Beauchamp, Boogaard, Topor-Stanley, Rose, McGlinchey (Grant 62), Emerton (Carrusca 84), Miller, Broich, Berisha.

MAN UNITED: Lindegaard, Rafael, Ferdinand (Keane 46), Jones, Evra (Fabio 75), Zaha, Carrick (Anderson 71), Cleverley, Lingard, Giggs (Van Persie 62), Welbeck (Januzaj 71).

REFA: Toma Masaaki [Japan]

MAGOLI:

A-LEAGUE ALL STARS IX 1

-Berisha Dakika ya 52

MAN UNITED 5

-Jesse Lingard Dakika ya 11 & 55

-Danny Welbeck 34 & 70

-Van Persie 87

MANCHESTER UNITED==ZIARA:

Julai 13 Singha All Star 1 Man United 0

Julai 20 A-League All Stars 1 Man United 5

Julai 23 Yokohama F-Marinos (Nissan Stadium,Yokohama) [Saa 7.20 Mchana]

Julai 26 Cerezo Osaka (Osaka Nagai Stadium, Osaka) [Saa 7 Mchana]

Julai 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong) [Saa 9 Mchana]

Agosti 6 AIK Fotboll (Friends Arena, Stockholm)

Agosti 9 Sevilla (Old Trafford - Rio Ferdinand Testimonial) [Saa 3.30 Usiku]

KIKOSI CHA MAN UNITED KWENYE ZIARA:

MAKIPA: David de Gea, Anders Lindegaard, Ben Amos

MABEKI: Rio Ferdinand, Jonny Evans, Phil Jones, Michael Keane, Rafael, Fabio, Alexander Buttner, Patrice Evra

VIUNGO: Michael Carrick, Tom Cleverley, Anderson, Ryan Giggs, Wilfried Zaha, Jesse Lingard, Adnan Januzaj

MAFOWADI: Danny Welbeck, Robin van Persie

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top